Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WADAU WA MAENDELEO KUSHIRIKIANA NA BARAZA KUTOKOMEZA MALARIA NCHINI 2030

Posted on: July 1st, 2023

Na. WAF- Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Baraza la Kutokomeza Malaria Tanzania, Leodigar Tenga ametoa wito kwa wajumbe wa baraza kuwa karibu na wadau wa maendeleo wa afya kwa ajili ya kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030.

Bw. Tenga ametoa rai hiyo leo katika ziara ya Baraza hilo walipotembelea kiwanda cha Viuadudu Kibaha Mkoani Pwani na kujionea shughuli zinazofanyika katika kiwanda hicho.

Tenga amesema ili kufanikisha kutokomeza malaria nchini jamii inapaswa ipatiwe elimu sahihi ya matumizi ya afua mbalimbali ikiwemo matumizi ya viuwadudu katika kuharibu mazalia ya mbu katika mazingira.

Aidha, Tenga ametoa Rai kwa Serikali kuhakikisha halmashauri zote nchini hususani zenye kiwango kikubwa cha Malaria kununua na kutumia viwadudu vinavyotengenezwa katika kiwanda cha Tanzania Biotech Product Limited.

Kwa upande wake Mmoja wa Wajumbe wa Baraza hilo, Faraja Kotta Nyalandu amesema kuwa ziara hiyo imekuwa chachu kwao kwani amejifunza na kuona nafsi ya dawa katika vita vya kutokomeza malaria nchini.

Lakini pia ameeleza kuwa kuna dawa zinatengenezwa hapa nchini ambazo zinaweza tumika kuharibu mazalia ya mbu na kufanya Tanzania kuwa salama juu ya malaria kwa kuua mazalia ya mbu kabla haja sambaza vimelea kwa mtu.

“Tumepata chachu ya kubuni mikakati itakayo saidia kujibu changamoto za sehemu husika katika vita dhidi ya malaria Tanzania ambapo tunaona maeneo yenye kiwango cha juu cha maambukizi ya malaria afua zake haziwezi kuwa sawa na maeneo yaliyonakiwango cha chini “. Amesisitiza Nyalabdu.

Vile vile, ameelezea kuwa wamepata elimu juu ya kudhibiti wa mazalia ya mbu huku akiitaka jamii kuchukua tahadhari dhidi ya malaria kwa kutumia chandarua na kupima ili kujua afya.