VIONGOZI WA KATA, WAHUDUMU WA AFYA 170 NGAZI JAMII WAPIGWA MSASA
Posted on: August 12th, 2024
NA WAF, Kilimanjaro
Viongozi wa Kata na Wahudumu wa afya ngazi ya jamii, wapatao 170 wamepatiwa elimu ya kujikinga na maradhi ili kuisaidia jamii kuepukana na maradhi mtambuka na kuwa na afya njema.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel Agosti 11, 2024 wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo viongozi hao mkoani Kilimanjaro
Dkt. Mollel amesema kuwa ni muhimu kwa viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kushirikiana ili kuhakikisha usalama wa afya za wananchi kwenye maeneo yao zinaimarika.
Awali akifungua mafunzo hayo Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe Ummy Nderiananga amewaasa viongozi na watumishi hao kuibua kwa Pamoja ikiwa kuna wagonjwa waliofichwa ndani ama walemavu kwani wote wanahaki ya kupata huduma za afya.
“Viongozi wa Kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii mna jukumu la kuwaibua watu waliofichwa, ili wapate msaada”. Amesema Mhe. Nderiananga.
Kwa Upande wake mkurugenzi wa operesheni na programu kutoka shirika lisilo la kiserikali la Apotheker Dkt. Angel Dillip amesema muda wa kuwaunganisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii na viongozi wa kata kutaimarisha hali ya huduma za afya kwa wananchi endapo watakua Pamoja.
Hata Hivyo Mkurugenzi wa Mipango, maendeleo ya Biashara na Sera kutoka Apotheker Dkt. Suleiman Kimatta amewaasa viongozi wa kata na wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kuweza kukabiliana na udumavu