Customer Feedback Centre

Ministry of Health

UJENZI WA HOSPITALI YA WATOTO KULETA MAPINDUZI MAKUBWA KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA KWA WATOTO

Posted on: July 29th, 2023

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa wito kwa Uongozi wa Hospitali ya watoto ya Rainbow kuwekeza nchini Tanzania ili kuongeza huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto nchini.

Waziri Ummy amesema hayo mjini Hyderabad alipofanya mazungumzo na uongozi huo katika kuimarisha ushirikiano ya huduma za kibingwa za magonjwa ya watoto nchini.

Aidha Waziri Ummy ameuomba Uongozi huo kuanzisha huduma za PICU (Paediatric Intensive Care Unit) na NICU (Neonatal Intensive Care Unit) katika kila hospitali ya wilaya au Halmashauri ili huduma hii ya watoto ipatikane kwa urahisi kwa wananchi.

Wazir Ummy amesema kuwa, katika kuimarisha ushirikiano na Taasisi hii ambayo ni maalumu kwa ajii ya kutoa huduma za watoto nchini India, serikali itaandaa hati ya mashirikiano (MoU) yenye lengo la kuuiarisha huduma za kibingwa za watoto nchini.

Hata hivyo Uongozi wa Hospitali ya Rainbow umeahidi kushirikiana na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika kufanya kambi za mara kwa mara za upasuaji ili kuhudumia watoto.