Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TUTAKUWA MSTARI WA MBELE VITA DHIDI YA MALARIA HADI TUFIKE 8%

Posted on: April 22nd, 2024

Waandishi wa Habari Mkoa wa Tabora wadhamiria kufanya kampeni kukabiliana na Ugonjwa wa Malaria na kushusha kiwango cha maambukizi hadi asilimia 8 kutoka Asilimia 23.4 ya sasa.

Wakizungumza wakati wa Semina ya Siku moja Aprili 22,2024 Mkoani hapo wao kama wadau wa maendeleo wa mkoa wa Tabora wanasikitishwa na kiwango cha sasa kinacho ufanya mkoa huwa kuongoza kwa maambukizi ya juu.

Akizungumza kwenye Semina hiyo, Dotto Elias ambaye ni Mwakilishi wa Shirika la Habari la Taifa (TBC) amesema nilazima kila mwanahabari wa mkoa huo awiwe kuona ukumbwa wa tatizo na kuiunga mkono Serikali kuhakikisha kiwango hicho kinashuka.

"Mmesikia hapa wenzetu wa Manyara wapo asilimia 0% kwa nn sisi Tabora tushindwe,? Amehoji Dotto.

Naye Paul Christian Kagenzi, Mwandishi wa Redio Uhai mkoani humo, amesema ajenda yakushusha Malaria sio ajenda ya Serikali bali kila mtanzania mwenye mapenzi mema.

"Ifahamike kuwa Malaria inaongoza kwakukwamisha shughuli nyingi za maendeleo hata kusababisha hasara ya asilimia 1% katika pato la Taifa, hii haina taswira nzuri ni vema tuuunganishe nguvu kwakuwa na vipindi vya elimu kwa umma maslahi mapana ya nchi yetu.