Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TANZANIA NA UINGEREZA KUSHIRIKIANA KATIKA TAFITI, MAFUNZO NA TIBA

Posted on: May 18th, 2023

Na. WAF - Dar Es Salaam

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeingia mkataba wa mashirikiano na Serikali ya Uingereza Katika sekta ya afya kupitia kwa Watanzania waishio Uingereza (Diaspora).

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe ameyasema hayo leo wakati wa hafla ya kusaini mkataba huo iliyofanyika katika ofisi ndogo ya Wizara Jijini Dar es salaam.

Dkt. Shekalaghe amesema ushirikiano huo unalenga katika maeneo ya Utafiti, Mafunzo, Tiba na shughuli zingine zote zinazo endana na Afya.

"Huu ni mkataba wa kwanza wa mashirikiano kati ya Wizara ya Afya na nchi ya Uingereza katika sekta ya afya ambayo ni hatua muhimu sana na haya ni matunda ya matokeo ya ziara ya mkutano wa Tanzania UK Health Summit.” Amesema Dkt. Shekalaghe

Aidha, Dkt. Shekalaghe amesema jambo lingine ambalo limezungumzwa katika mashirikiano hayo ni nchi ya Uingereza kuingia katika mfuko wa pamoja wa (Health Basket Fund) wenye lengo la kuwezesha kutoa huduma za afya ya msingi.

"Tumeisha tengeneza timu ya waatalam wetu kutoka Wizara ya Afya ambao watakaa na wataalam waliopo kwenye Balozi ili ihakikishe kuwa Uingereza ni mojawapo ya nchi ambayo itaweza kuchangia". Amesema Dkt. Shekalaghe

Kwa upande wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Dkt. David Concar amesema mkataba huu wa mashirikiano wa afya utaimarisha zaidi ushirikiano kati ys nchi hizi mbili.

"Tutafanya kazi kwa ushirikiano na Serikali ya Tanzania kusaidia uimarishaji wa mfumo wa afya, huduma za afya kwa wote na kupunguza vifo vya akina mama na watoto wachanga vinavyoweza kuzuilika." Amesema Dkt. Concar