Customer Feedback Centre

Ministry of Health

SERIKALI KULETA UNAFUU GHARAMA ZA USAFISHAJI FIGO

Posted on: August 2nd, 2023

Serikali imesema itahakikisha gharama za usafishaji figo zinakuwa nafuu ili kuokoa maisha ya watanzania.

Kauli hiyo imebainishwa na Waziri wa Afya, Mhe.Ummy Mwalimu
wakati akitoa ufafanuzi kufuatia hoja ya mmoja wa wananchi katika mtandao wa Twitter.

Waziri Ummy amesema kuwa huduma za kusafisha figo kwa wengine ni biashara ya faida kubwa lakini Serikali itahakikisha huduma hiyo ni ya gharama nafuu ili kuokoa maisha ya wengi

“Ni sahihi kabisa gharama za kusafisha figo nchini zipo juu sana wastani wa dola za Marekani 100 (sawa na Tshs 250,000) kwa awamu moja India ni kama dola za Marekani 30 (sawa na Tshs 74,000) kwa siku ambapo hata hiyp hata hiyo dola 30 kwa siku bado ni kubwa sana kwa watanzania wengi ambayo ni kama sh. 600,000 kwa mwezi bado wananchi wengi hawawezi kumudu”, amefafanua Waziri Ummy.

Ameeleza kuwa gharama hizo kubwa zinahatarisha uhai wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na inaweza kuzidiwa na gharama jubwa za dialysis. hivyo kuwakaribisha Wadau ambao wapo tayari kushirikiana nasi kufikia azma hii tutaendelea nao.

“Serikali itaendelea kuboresha huduma za usafishaji figo na kuwekeza zaidi kwenye huduma hizi ili mwananchi ataweza kumudu gharama hizo, tunawakaribisha wadau ambao wapo tayari kushirikiana nasi kufikia azma hii tutaendelea nao” amesisitiza Waziri Ummy.

Katika kuboresha huduma za usafishaji figo, hadi mwezi Machi 2023, Serkali kupitia Bohari kuu ya Dawa ilikuwa imekamilisha ununuzi wa mashine za dialysis 140 ambazo tayari zimesambazwa kwenye vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya nchini.