Customer Feedback Centre

Ministry of Health

SERIKALI KUENDELEA KUKABILIANA NA UNGONJWA WA KIFAFA

Posted on: February 12th, 2025

Na WAF,

Naibu Waziri wa Afya, Mhe. Godwin Mollel amesema Serikali itahahakikisha inaboresha miundombinu ya afya ili kukabiliana na ugonjwa wa kifafa, ambao huchukua asilimia 60 ya magonjwa ya afya ya akili.

Dkt. Mollel amesema hayo Februari 10, 2025 wakati wa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya ugonjwa wa Kifafa Duniani kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Dkt. Mollel amewataka watumishi wa afya nchini kufanyakazi kwa juhudi zote na kusiwepo na eneo lolote ambalo limeachwa nyuma kwenye utoaji huduma ya afya kwa wagonjwa wa kifafa kwa sababu teknolojia nyingi zimepelekwa katika hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma.

Dkt. Mollel amesema jamii kwa ujumla inatakiwa kuweka desturi hasa kwa wakazi wa maeneo ya vijijini, kuwa kila wanapokutana katika vikao vya kimaendeleo basi waweke ajenda ambayo itakuwa ni desturi yao kuzungumzia kifafa ili iwe rahisi na haraka kupata taarifa za wagonjwa hao.

Kwa upande wake Bw. Isrey Athuman, amemshukuru Dkt. Mollel kwa msaada wa kumpatia dawa za mwaka mzima kutokana na tatizo lake hilo la kifafa pamoja na kumuendeleza kielimu ili aweze kupata ajira itakayo mwezesha kujikimu kimaisha.

Dkt. Mollel ametumia fursa hiyo kuiasa jamii kujenga tabia ya upendo na kuacha kuwanyanyapaa watu wenye tatizo hili ili wasijione wakiwa na watu wasio na mchango ndani ya jamii.