Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RAIS SAMIA APUNGUZA RUFAA ZA MATIBABU YA NJE YA NCHI KWA ASILIMIA 97

Posted on: September 23rd, 2023

Na. WAF, Kibaha


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya kwa kupunguza Rufaa za nje ya nchi kwa asilimia 97.


Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwini Mollel wakati alipo mwakilisha Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kutengeneza vitendanishi Action Medeor Mkoani Kibaha


Dkt. Mollel kuwa amesema Rais Dkt. Samia ametoa kiasi cha shilingi Tirioni 6.7 ili kuboresha Huduma za afya nchini kwa kuwezesha upatikanaji wa viafaa tiba, dawa na vitendanishi, uboreshaji wa miundombinu, kuongeza wataalamu wa afya na kusomesha waataalam kupitia programu ya Samia Scholarship.


Uboreshaji huo umefanya mapinduzi makubwa nchini kwa kuleta matokeo chanya na kufanya hospitali za rufaa za mikoa zote nchini kuwa na uwezo wakutoa Huduma ya CT Scan na hakuna hajaa ya rufaa ya Huduma hizo katika mkoa husika


Amesema kuwa majengo ya Huduma za dharura 128 na majengo ya wagonjwa maututi 78 yamejengwa kwa mwaka 2023 hivyo ni jukumu la wataalamu wa afya kuhakikisha wanavitunza vifaa tiba vizuri ili kuwahudumia wananchi katika ubora unao stahili.


“Dhamira ya Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kufanya kazi yenye kuleta matokeo chanya kwa wananchi kwa kuhakikisha afya za watanzania ziko salama na imara ili kuendelea na shughuli zao za kutafuta kipato”, ameeleza Dkt. Mollel


Dkt. Mollel amesema kuwa leo Tanzania kanda zote zina Mashine ya MRI mbili kwa ajili ya kutoa Huduma katika kanda hizo na mashine moja ni Bilioni 3.


Aidha Dkt. Mollel amewataka TMDA na MSD kuhakikisha wanafika katika kiwanda hicho na kutatua changamoto zilizopo ili kuwezesha kiwanda hicho kufanya uzalishaji kwa ufasaha.


“Kiwanda cha Action Medeor kitazalisha dawa na kuuza kwa shilingi 80,000 hivyo kitasaidia sana serikali kuokoa fedha kwani awali tulikuwa tunanunua vitendanishi hivyi kwa shilingi 320,000”, ameongeza Dkt. Mollel


Vile vile amewapongeza chuo cha DIT kwa ubunifu, maarifa na teknalojia katika sekta ya afya ili kufikia utoaji wa Huduma b ora kwa wananchi.