Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RAIS SAMIA AMEFANYA MAGEUZI MAKUBWA NDANI YA SEKTA YA AFYA NCHINI:

Posted on: April 27th, 2024


Na WAF,Tabora


Naibu Waziri wa Afya, Dkt Godwin Mollel amesema Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya afya kwa kuwekeza kwenye, teknolojia, Elimu, wataalamu, kupeleka huduma karibu na wananchi na ununuzi wa vifaa tiba vya uchunguzi.


Akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu, Dkt. Dotto Biteko Aprili 27, 2024 mkoani Tabora wakati wa Maadhimisho ya kilele cha miaka 25 ya huduma ya maendeleo ya mtoto na kijana nchini yaliyoandaliwa na shirika la Kimataifa la Compassion.


Dkt . Mollel amesema Rais Dkt. Samia m anawapenda sana watanzania ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu, tiba, technolojia na utaalamu waliokuwa wakiufuata nje ya Nchi wamezileta kwa asilimia 97.


Amesema ilikuwa ukienda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili miaka minne iliyopita ukiwa unatatizo la moyo unafunguliwa kifua kizima.


"Lakini Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuja Muhimbili tukamwambia tuna shida maana watu wanakaa wodini na ugonjwa wa moyo unaleta gharama katika jamii kwa kukaa muda mrefu”, ameeleza Dkt. Mollel.


Ameongeza kuwa zaidi ya bilioni 28 zimetolewa kununua vifaa tiba ambapo mgonjwa akiingizwa katika mashine hakuna haja ya kufungua kifua na baada ya muda mfupi anaruhusiwa kurudi nyumbani.


"Tunaingia kwenye mshipa mkubwa hapa mguuni tunaelekea kwenye moyo tunakupiga operationi baada ya siku mbili unaelekea kwako una enda nyumbani," amesema Dkt. Mollel. 


Aidha amesema kuna wagonjwa wengi walikuwa wakipelekwa nchini India kwenda kutibiwa na fedha nyingi zilikuwa zikitumika kwa matibabu huko nje ya nchi.


Ameongeaza kuwa, kwenye ugonjwa wa Selimindu Rais Samia ameleta technolojia ya kutibu ugonjwa huo.


"Leo pale Hospitali ya Kanda ya Rufaa ya Benjamini Mkapa tunachukua kitu kwenye mifupa kwa ndugu yako ambaye hana tatizo hilo unapandikizwa unapona”, ameeleza .


Dkt. Mollel amesema kuna waliokuwa wakizaliwa wanavibyongo ambapo Rais Samia amenunua mashine maalumu ambayo imetatua changamoto hiyo.


Vile vile ameongeza kuwa kuna kiwanda cha kuzalisha mionzi tiba ambapo kwa Afrika ni Nchi tano pekee ndio zenye kiwanda kama hicho kwa sababu ya gharama kuwa kubwa na kiwanda hicho kimesaidia kuzalisha mionzi tiba ambayo ilikuwa ikitoka nje ya Nchi.


Pia ameongeza kuwa Tanzania inauwezo wa kugundua ugonjwa wa kansa kabla ya miaka mitano kutokana na uwepo wa mashine za kisasa zilizowekezwa na Rais Samia.


Amesema teknolojia hizo zimeshuka mpaka katika ngazi ya Zahanati kwani wengi waliokuwa katika Hospitali ya Ocean Road walikuwa katika hali mbaya.


"Lakini juzi tumeenda na kamati ya Bunge asilimia 70 wamepatikana na hatua ya kwanza wanatibiwa na watapona," amebainisha Dkt .Mollel


Amesema kwa miaka mitatu Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitegemea kufikisha vifo vya kina mama wafikishe 250 mwakani kati ya vizazi hai 100,000 lakini kwa uwekezaji wa Rais Samia ile trilioni 6.6 ikashuka mpaka katika ngazi ya Zahanati.


Amesema Serikali ya awamu ya sita imewekeza kwenye wataalamu,kupeleka huduma karibu na wananchi,kuwekeza kwenye elimu na teknolojia.


Mwisho.