Customer Feedback Centre

Ministry of Health

NCHI WANACHAMA WA WHO KANDA YA AFRIKA ZAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA UCHUNGUZI WA MAGONJWA NA MAABARA

Posted on: August 30th, 2023

Na WAF, Gaborone - Botswana


Nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) kanda ya Afrika zimekubaliana kuboresha huduma za uchunguzi wa Magonjwa na Maabara ambapo TANZANIA imefanikiwa kusimika vifaa vya maabara 2,357 sehemu mbalimbali ikiwemo ngazi ya Afya ya Msingi na Rufaa ambavyo ni MRI Saba, CT-Scan 32 na mashine za X-ray 179 pamoja na na vifaa mchanganyiko vya maabara nchini. 


Waziri Ummy ameyasema hayo leo Agosti 30, 2023 wakati akiendelea kushiriki kikao cha Mawaziri wa Afya wa Nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Àfrika kinachoendelea mjini Gaborone, Botswana.


“Kikao chetu cha leo tarehe 30.08.23 tumejadili kwa kina mkakati wa kikanda wa huduma za uchunguzi, utambuzi na matibabu ya magonjwa kwa kuimarisha huduma za maabara na mionzi”, amesema Waziri Ummy 


Aidha, Mhe. Ummy ameueleza mkutano huu wa 73 wa WHO Kanda ya Afrika kwamba, Tanzania imefanikiwa na kutekekeza kwa vitendo Mkakati huo, hivyo kutokana na ongezeka la vifaa vya uchunguzi wa magonjwa vinavyohitaji matunzo na matengenezo.


“Kufuatia uhitaji huo Serikali imeajiri wataalamu wa vifaa tiba 150 ili kusaidia katika matengenezo kinga ya vifaa tiba pamoja na kujenga karakana Sita ngazi ya Kanda”, amesema Waziri Ummy


Pia, Waziri Ummy amesema kufuatia kuimarisha ubora wa huduma za uchunguzi wa magonjwa na huduma za maabara, Tanzania imefanikiwa 

Kupata ithibati za kimataifa katika maabara 61 za kawaida na maabara za vituo vya Damu Salama kwenye Kanda mbalimbali za nchini Tanzania.


Wakichangia mada hiyo, wajumbe wa mkutano huo wameeleza kuwa, hawaridhishwi na kasi ya utekelezaji wa mkakati huo kwa sababu iliyoelezwa kuwa ucheleweshwaji wa utekelezaji wa mkakati huu ni ukosefu wa rasilimali fedha, ukosefu wa miundombinu, rasilimali watu, ukosefu wa vifaa wezeshi kwa nchi wanachama ambapo wameshauri kuwa nchi husika na washirika wakuu katika eneo hili waongeze uwekezaji wa rasilimali fedha katika eneo hili ili kuhakikisha mkakati huu unatekelezwa kikamilifu na kwa wakati. 


Vilevile, nchi wanachama wameitaka WHO Kanda ya Afrika kutoa msaada wa kitaalamu (Technical Support) kwa nchi wanachama ili kuharakisha utekelezaji wa mkakati huu kwa uwiano.