Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MAFUNZO YA UBORA WA HUDUMA YATOLEWA KWA WAGANGA WAFAWIDHI WA HOSPITALI ZA MIKOA

Posted on: August 27th, 2022Na WAF- MWANZA

WIZARA ya Afya kupitia Idara ya tiba imetoa mafunzo ya kuboresha utoaji huduma kwa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa zote nchini ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Wizara ya kuhakikisha mwananchi anapata huduma za afya bora.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika Jijini Mwanza yamemalizika leo Agosti 27, huku kwa pamoja wakikubaliana kusimamia huduma bora kwa wananchi, hasa kutokana na Serikali kuboresha miundombinu, upatikanaji wa vifaa na vifaa tiba katika hospitali hizo.

Akifunga mafunzo hayo, Mkurugenzi Msaidizi anaesimamia Hospitali za Rufaa za Mikoa Dkt. Caroline Damian amesema, lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo viongozi wa Hospitali hizo ili waweze kusimamia vyema huduma zote zinazoendelea katika maeneo yao ili mwananchi aweze kunufaika.

"Lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo viongozi katika ngazi ya Hospitali za Rufaa za Mikoa ili waweze kusimamia afua zote wanaotakiwa kuzitekeleza katika ngazi ya hospitali zao." Amesema Dkt. Caro.

Pia, Dkt. Caro amesema, kundi lingine lililonufaika na mafunzo hayo ni pamoja na Wauguzi wafawidhi, Maafisa Utumishi, Waratibu wa ubora wa huduma, Waratibu wa huduma za tiba katika hospitali pamoja na Wahasibu ambao watasaidiana na viongozi wengine katika hospitali za mikoa ili kuleta matokeo chanya katika Sekta ya Afya.

Aidha, Dkt. Caro ametoa wito kwa viongozi wote walioshiriki mafunzo hayo kwenda kutekeleza makubaliano waliojiwekea ili kufikia adhma ya Serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi wa hali zote, na kuondoa kero na malalamiko yanayoweza kuzuilika katika maeneo ya kutolea huduma.

Nae, Mwakilishi wa Waganga Wafawidhi wa Hospitali za Rufaa za Mikoa, ambaye pia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Amana Dkt. Bryceson Kiwelu amesema, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Sekta ya Afya ikiwemo miundombinu na vifaa tiba, hivyo mafunzo hayo yataongeza tija kwenye utoaji huduma bora kwa wananchi.

"Serikali ya awamu ya sita imefanya uwekezaji mkubwa sana katika Sekta ya Afya, tumeona miundombinu imeboreshwa, vifaa tiba vimenunuliwa kama CT-SCAN, Digital X-ray pamoja vingine,