Customer Feedback Centre

Ministry of Health

KAMBI YA KUPIMA AFYA BURE (AFYA CHECK) KUTUA TANGA MJINI

Posted on: August 14th, 2023

Taasisi ya Afya Check kwa kushirikiana na Mbunge wa Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu na Halmashauri ya Jiji la Tanga imeandaa kambi maalumu ya wananchi kupima afya zao bure ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia za kusogeza huduma za Afya kwa wananchi.

Wakiongea katika Mkutano na Vyombo vya Habari, Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga leo tarehe 14/Agosti 2023 Mbunge wa Tanga Mjini ambae pia ni Waziri wa Afya Mhe UMMY MWALIMU amesema kuwa Kambi hiyo itafanyika katika Viwanja vya Usagara Sekondari Tanga kuanzia tarehe 21 hadi 25 Agosti 2023.

Huduma zitakazotolewa ni kupima Pressure (Shinikizo la Damu), Kisukari, Macho na kupima aina tatu za Saratani ambazo ni Saratani ya matiti, saratani ya Mlango wa Kizazi na Tezi Dume. Na kuhusu kupima Tezi dume Mhe Ummy amewataka wanaume kutoogopa kwa kuwa kipimo kitakachotumika ni kipimo rafiki.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Afya Check Dkt ISAAC MARO ameeleza kuwa Taasisi ya Afya Check inaendesha kambi hizi ili kuwajengea wananchi utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwa lengo la kujikinga na kudhibiti magonjwa hasa magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Hadi sasa wameshaendesha Kambi zaidi ya 10 za Kupima Afya katika Mikoa mbalimbali nchini, Kambi ya mwisho ilifanyika mkoani Dar es salaam mwezi Julai 2023.

Nae Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga, Mhe ABDURAHMAN SHILLOO amempongeza Mhe Ummy kwa jitihada zake nyingi na za mara kwa mara za kuwatumikia watu wa Tanga Mjini. Aidha amewahakikishia Afya Check kuwa Halmashauri ya Jiji la Tanga itatoa ushirikiano wote ili kufanikisha kambi hii yenye manufaa kwa watu wa Tanga.

Akiongea kwa niaba ya Mfadhili Mkuu wa Kambi hizi, Benki ya CRDB bwana SAMSON KEENJA alieleza kuwa Benki ya CRDB inaunga mkono jitihada za serikali za kusogeza huduma za Afya kwa wananchi ikiwemo kuwezesha wananchi kupima Afya.

Pia wamemshukuru Rais dkt Samia kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara ili kukuza uchumi.

Mkutano huu pia umehudhuriwa na Kamati ya Uendeshaji Afya Mkoa (RHMT) ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Japhet Simeo,