Customer Feedback Centre

Ministry of Health

JENGO LA MAMA NA MTOTO HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SIMIYU LAKAMILIKA KWA ASILIMIA 95

Posted on: February 23rd, 2024



Na: WAF, Simiyu

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu imekamilisha ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto kwa asilimia 95 ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuboresha huduma za afya ya Mama na Mtoto kama Kipaumbele cha Sekta ya Afya.

Hayo yamejiri kufuatia ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dkt. Grace Magembe Mkoani Simiyu wakati wa Ukaguzi wa Miradi ya ujenzi ya Hospitali na utoaji wa huduma za afya

Jengo hilo likikamilika litakuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 140 vya kuhudumia wajawazito na watoto. Hii ni habari njema kwa wananchi wa Simiyu, kwani jengo hili litasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuboresha afya ya jamii kwa ujumla.

"Manufaa ya jengo hili ni pamoja na kupunguza gharama na muda wa kusafiri kwa wagonjwa, kuongeza upatikanaji wa huduma za afya, na kuboresha afya ya uzazi na watoto". Amesema Dkt. Magembe

Aidha Dkt. Magembe amesema kukamilika kwa jengo hili ni hatua muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu kuhusu afya ya uzazi na mtoto, na inaonyesha dhamira ya serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.