Customer Feedback Centre

Ministry of Health

HOSPITALI YA WILAYA TEMEKE, KUJENGWA VIKURUTI CHAMAZI

Posted on: August 11th, 2023

Na. WAF - Dar es Salaam

Serikali inatarajiwa kujenga Hospitali ya Wilaya ya Temeke katika eneo la Vikuruti lilipo Chamazi, Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mkoani Dar es Salaam ilikupunguza msongamano katika vituo vya Afya vilivyo ndani ya Temeke.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya kukagua utoaji wa huduma za Afya katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambapo amesema kuwa watu wamekuwa wakiongezeka hivyo vituo vya huduma vimezidiwa hali ambayo wanaonelea kupanua huduma kwa kuja na Hospitali hiyo.

“Rais Dkt. Samia amenielekeza niwaelekeze Hospitali ya Taifa Muhimbili - MUHAS kutoa ekari 30 kuipatia Manispaa ya Temeke pale Vikuruti ili kujengwa Hospitali nyingine ya Wilaya kubwa nzuri”, amesema Waziri Ummy

Amesema, Manipaa ya Temeke inaongezeko kubwa la watu takribani Milioni 1.6 lakini kukiwa na uhaba wa Vituo vya kutolea huduma hivyo tumeamua kama Serikali kujenga Hospitali ya Wilaya.

Hospitali hii ya Wilaya ya Temeke tutaijenga Vikuruti-Chamazi itasaidia zaidi kupunguza mzigo wa wananchi kufuata huduma maeneo ya hizi hospitali ya Temeke na Mbagala Rangi Tatu.’’ Amesema Waziri Ummy Mwalimu.

Awali akipokea taarifa juu ya huduma za Afya ndani ya Temeke, Waziri Ummy amewaomba watendaji wa Temeke kuhakikisha wanatafuta maeneo ilikuweza kujengwa vituo vya Afya.

“Mhe Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hashindwi, nyie tafuteni maeneo tutakaa sisi Wizara ya Afya na TAMISEMI kuona namna ya kupata maeneo ya kuweza kujenga hivi Vituo vya Afya ilikuweza pia kupata Vituo vya Afya.