Customer Feedback Centre

Ministry of Health

DKT. MPANGO AELEKEZA WANAOHUSIKA NA WIZI WA VIFAA TIBA WATAFUTWE POPOTE WALIPO NA WACHUKULIWE HATUA

Posted on: May 17th, 2023

Na WAF- Karatu.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango ameelekeza kutafutwa kwa watu wote wanaohusika na wizi wa vifaa tiba popote waliopo na hatua kali zichukuliwe dhidi yao kwani ubadhilifu huo unawakosesha wananchi haki yao ya msingi ya kupata huduma za afya bora katika maeneo yao.

Dkt. Mpango amesema hayo Mei 16, 2023 wakati  akifungua rasmi hospitali ya Wilaya ya Karatu iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.37, na kuongea na wananchi, watumishi pamoja viongozi mbalimbali waliojitokeza katika tukio hilo katika Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.

Amesema, "Napenda niongeze sauti yangu, sehemu ya hii fedha ni kodi yenu... sina lugha nyepesi kwa hao, hao ni wahujumu watafutwe, wasakwe, wakamatwe popote walipoiba sio hapa peke ake, wanaturudisha nyuma... ndugu zangu wa Karatu hospitali hii ni kitu kizuri kwenu, tunaomba muitunze na msiruhusu mambo ya namna hii." Amesema Dkt. Mpango.

Ameendelea kusema kuwa, Serikali itaendelea kuhakikisha huduma bora za afya zinasogezwa karibu zaidi na wananchi pamoja na kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika kila vituo vya kutolea huduma za afya.

Aidha,  Dkt. Mpango ameagiza uongozi wa Wilaya na hospitali kusimamia kwa uaminifu dawa zinazoletwa na Serikali kwa ajili ya matumizi ya wananchi ambapo kinyume na hapo Serikali itachukua hatua kali za kisheria dhidi ya kiongozi yeyote atakayebainika kukiuka sheria na miongozo iliyotolewa na Serikali ya uendeshaji wa maduka ya dawa ya hospitali.

Sambamba na hilo, amesema, hospitali hiyo inalenga kusaidia watalii kuwa na uhakika wa kupata huduma ya kwanza na ya dharura kwa haraka katika mazingira salama pale itakapo hitajika.

Vilevile Dkt. Mpango ametoa wito kwa watoa huduma wa afya katika hospitali hiyo, kuwahudumia wananchi kwa upendo na uadilifu, pia kufuata miongozo, miiko, maadili na viapo vyao wakati wote wa utoaji huduma.

Amesema, Serikali itaendelea kuhakikisha vitendea kazi vinapatikana ili majengo yote yaanze kufanya kazi kama ilivyokusudiwa, huku, akitoa wito kwa wananchi, kushirikiana na uongozi wa Wilaya