Customer Feedback Centre

Ministry of Health

DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO 2050 BIMA YA AFYA KWA WOTE ITAKUWA CHACHU KUBOREHA HUDUMA ZA AFYA: MHE. UMMY

Posted on: July 6th, 2024

Na WAF, DSM


Waziri wa Afya Mhe.Ummy Mwalimu ameiasa tume inayopokea maoni kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa 2050 suala la Bima ya Afya kwa wote liwe kipaumbele ili kuzidi kuboresha huduma za Afya.


Mhe. Ummy amesema kote ulimwenguni gumzo kwa sasa ni Afya kwa wote hivyo Tanzania kama nchi hatunabudi kuingiza suala la Bima ya Afya kwa wote katika Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050.


Mhe. Ummy ameyasema hayo Leo Julai 06, 2024 wakati wa Kongamano la kitaifa la wadau wa Sekta ya Afya kuhusu maandalizi ya Diara ya Taifa ya Maendeleo 2050.


"Ndugu zangu watanzania kama kila mmoja wetu akiguswa na kuchangia huduma za Bima ya Afya ni dhahiri shahiri kuwa huduma zetu zitaboreka" amesema Waziri Ummy.


"Tusingoje mgonjwa yupo, Mujimbili, JKCI, Bugando au mahala pengine ndio uanze kukimbizana na Bima ya Afya, hakuna Bina ya hivyo, tuzingatie miongozo na Sheria inavyotaka" amesema Mhe.Ummy 


Katika hatua nyingine Waziri Ummy amesema, Wizara ya Afya imefanya vizuri katika Dira ya 2000/2025 inayomaliza muda wake katika masuala kadha mbali yakukabiliwa na baadhi ya magonjwa ya mlipuko kama Kovidi 2019.


"Tumefanikiwa sana, juu ya suala la wanawake kujifungulia katika Vituo vya Afya, kwani imeongezeka kutoka asilimia 41 mwaka 2000 hadi kufikia asilimia 81 kwa sasa na tutajitahidi ifikapo 2025 tuwe tumefikia asilimia 100, amesema Mhe. Ummy 


Akifungua Kongamano hilo lililowashirikisha wadau wa Afya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo ameipongeza Wizara ya Afya kwakuandaa Kongamano hilo ikiwa ni wizara ya kwanza kufanya hivyo.


"Ninyi ndio mnao ijua Sekta ya Afya, mmeamua kuwaita wadau wenu waje watoe maoni yao, ili sisi iwe kazi yetu iwe rahisi, tunapo andaa Dira ya Taifa ya 2050" Amesema Prof. Kitila


Akitoa Salaam za Ofisi ya Rais TAMISEMI Naibu Waziri Dkt. Festo Dugange, aliiomba kamati inayopokea maoni kuzingatia suala la kuboresha huduma za Kibingwa katika ngazi ya msingi.


Kongamano la kitaifa la wadau wa Sekta ya Afya limeandaliwa na Wizara ya Afya na kuwaalika wadau wake kwa ajili yakutoa Maoni yatakayowezesha kuingizwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050 kwa mustakabali wa Afya za watanzania. 


MWISHO