WIZARA, MIKOA TISA WAJIPANGA KUPAMBANA NA KIFUA KIKUU
Posted on: January 9th, 2025
Na WAF, Dodoma
Waganga Wakuu wa mikoa tisa na Waratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa mikoa wameonesha utayari wao wa shughuli za uibuaji wa wagonjwa wa kifua kikuu kwenye mapango harakishi wa kuwaibua na kuwaweka katika matibabu wagonjwa wa Kifua Kikuu zaidi ya 14000 wakiwemo watoto.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Ahmed Makuwani Januari 8, 2025 wakati akifungua kikao kazi cha Waganga Wakuu wa mikoa, Waratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma wa mikoa na Wataalam wa Wizara ya Afya kujadili utekelezaji wa mpango harakishi wa uibuaji wagonjwa wa Kifua Kikuu.
Mpango huo unategemewa kutekelezwa ngazi ya vituo vya kutolea huduma za afya pamoja na ngazi ya jamii hususani makundi yaliyo maeneo hatarishi ya maambukizi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu kama vile wachimbaji wa madini, wavuvi, wadungaji sindano, wafungwa na makundi mengine katika mikoa tisa (9) na halmashauri 76 Tanzania Bara.
Dkt. Makuwani amesema Tanzania inaendelea kukabiliana na changamoto ya kuwapata wagonjwa wa Kifua Kikuu na kuwaweka kwenye matibabu ili kuiondoa nchi kwenye kundi la nchi 30 zinazochangia asilimia 87 ya wagonjwa wote wa Kifua Kikuu Duniani.
“Januari 6, 2025 Waziri wa Afya, Mhe. Jenista Mhagama alizindua rasmi mpango wa kitaifa wa kuharakisha uibuaji wa wagonjwa wa Kifua Kikuu katika mikoa tisa (9) ya Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Mara, Simiyu, Shinyanga, Ruvuma na Tanga na kugawa mashine 185 za ugunduzi wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu na alitoa maelekezo yanayolenga kuongeza juhudi za uibuaji wagonjwa wa Kifua Kikuu nchini,” amesema Dkt. Makuwani.
Dkt. Makuwani amesema, lengo ni kupunguza visa vya Kifua Kikuu kwa 50% na vifo kwa 75% ifikapo 2025 ikilinganishwa na takwimu za mwaka 2015, ambapo kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2023, Tanzania imeweza kupunguza visa vya Kifua Kikuu kwa asilimia 40.
“Tanzania imeweza kupunguza vifo vinavyotokana na Kifua Kikuu kwa asilimia 69 kwa takwimu za mwaka 2023, ambapo lengo ni kupunguza hadi kufikia asilimia 75