Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

WAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA JKCI KWA KUANZISHA HUDUMA ZA MOYO JIJINI ARUSHA

Posted on: January 28th, 2026

Na WAF, Arusha


Waziri wa Afya Mhe.Mohamed Mchengerwa amepongeza Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa kushirikiana na Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center maarufu kama Selian kwa kuanzisha huduma za uchunguzi na matibabu ya moyo kwa wananchi wa jiji la Arusha na Mikoa ya jirani.


Waziri Mchengerwa ametoa pongezi hizo Januari 27, 2025 wakati wa ziara ya kutembelea Hospitali hiyo iliyopo jijini Arusha ili kujionea namna huduma za moyo zinavyotolewa kwa wananchi.


Waziri Mchengerwa amesema huo ni muunganiko mzuri na mahsusi ukizingatia Taifa limepata nafasi ya kipekee ya kuandaa mashindano ya kimataifa ya mpira wa miguu barani afrika yajulikanayo kama AFCON 2027.


“Ameeleza Mkurugenzi hapa kuwa wameweka kituo maalum kinachojulikana kama Sports Cardiology Centre hapa katika hospitali hii. Kituo hiki ni maalum kwa ajili ya kutoa huduma za kibingwa na kibingwa bobezi maalum kwa wanamichezo wote watakaoshiriki mashindano haya kwa kufanya vipimo vyote muhimu kabla, wakati na hata baada ya mashindano”, amesema Waziri Mchengerwa.


Aidha, amesema kuwa tangu kuanza kwa ushirikiano huo mwezi Novemba mwaka 2025 jumla ya wagonjwa 11,051 wameshapata huduma za kibingwa za uchunguzi na matibabu ya moyo Selian, kati ya hao waliolazwa ni 482, jumla ya pasuaji kubwa na ndogo 1533 zimeshafanyika pamoja na wagonjwa 1297 wamepata huduma za utengemao (physiotherapy) katika kipindi hiki.


Akitoa Salaam za Wizara Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe amesema JKCI na Lutheran atakuwa tayari kuwapokea na kuwasikiliza jinsi walivyo jipanga katika suala zima la utoaji wa huduma.


Kwa Upande wake Mkurugenzi wa JKCI Dkt. Kisenge amesema tayari taasisi hiyo imefungua vituo sita kwenye Kanda mbalimbali nchini sambamba na kuwafikia watu zaidi 23,000 kwa huduma za moyo kote nchini kupitia huduma za Mkoba