Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

SERIKALI WEKENI MAZINGIRA RAFIKI KWA WAWEKEZAJI WA VIWANDA VYA DAWA; MHE. NYONGO

Posted on: February 19th, 2024


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI imeendelea kutoa wito kwa Serikali kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wa viwanda vya dawa ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa dawa nchini.


Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Masuala ya Afya na UKIMWI, Mhe. Stanslausi Nyongo wakati akihitimisha ziara ya kamati baada ya kutembelea viwanda vya kuzalisha dawa Mkoani Pwani


Mhe. Nyongo amesema kuwa viwanda vya dawa vikiwa vingi nchini itasaidia kupunguza kuwa tegemezi wa dawa kutoka kwa mataifa mengine.


“Kama Bunge limeishapitisha maamuzi ya kuitaka serikali kuweka mazingira mazuri kwa watanzania kuweza kuwekeza katika sekta ya afya ili kupambana na adui maradhi”, ameeleza Mhe. Nyongo


Ameendelea kushauri Serikali kuendelea kuwakaribisha wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha dawa, vifaa tiba na vitendanishi ili kuongeza upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini na nje ya nchi ili kuongeza fedha ya kigeni