WAZIRI JENISTA MHAGAMA AKABIDHIWA OFISI NA MHE. UMMY MWALIMU
Posted on: August 16th, 2024
Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Agosti 16, 2024 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.
Shughuli ya makabidhiano ya ofisi imefanyika Leo tarehe 16 Agosti, 2024 katika Ofisi za Wizara katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.
Mhe. Jenista amempongeza Mhe. Ummy Mwalimu kwa uongozi wake ndani ya Wizara ya afya kwa kipindi chote alichofanya kazi ndani ya Sekta ya Afya kwa miaka 14.
“Nakupongeza Mhe. Ummy Mwalimu hakika maendeleo haya ya Sekta ya Afya una mchango mkubwa katika kuifikisha Sekta ya Afya hapa ilipo, tutaendelea kushirkiana na kupeana ushauri zaidi katika kazi” amesema Waziri Mhagama.
Akikabidhi Ofisi Mhe. Ummy Mwalimu amempongeza Mheshimiwa Jenista Mhagama kwa kuaminiwa na kuchaguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa Waziri wa Afya.
“Umekuwa Kiongozi mwenye uzofu wa kutosha ndani ya Serikali naamini kwa uwezo wako ulionao pamoja na timu hii ya Wizara unaweza kuendelea zaidi katika kuboresha Sekta ya Afya nchini” amesema Mhe. Ummy Mwalimu.
Viongozi wengine wageni walioshiriki kwenye shughuli hiyo ni Naibu Katibu Mkuu Bw. Ismail Rutamila ambaye pia ameahidi kutoa ushirikiano kwa Menejimenti na Viongozi katika kuboresha Sekta ya Afya nchini pamoja na Dkt. Irene Isaka, Mkurugeni Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima