Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

UVIMBE ULIOMTESA KWA MIAKA 10 WATOLEWA NA MABINGWA WA RAIS SAMIA

Posted on: September 19th, 2024

Na WAF-Masasi 


Madaktari Bingwa wa  Samia Suluhu Hassan  wamefanikiwa kumtoa uvimbe wenye uzito wa gramu 800 kwenye kizazi mgonjwa alioishi nao kwa zaidi ya miaka 10.


Hayo yamebainishwa na Daktari Bingwa wa  Magonjwa ya wanawake na uzazi , Dkt. Emmanuel Imani Ngadaya kutoka Hospitali Rufaa ya Kanda ya kusini aliye ongoza  jopo  la Madaktari Bingwa wa Rais Samia Suluhu Hassan katika  Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu mkoani  Mtwara. 

mara baada ya kukalilika kwa upasuaji huo .


Dkt.  Ngadaya ameeleza kuwa wakiwa katika utekelezaji wa kampeni hiyo walipokea mgonjwa aliyekuwa na taizo la uvimbe kwenye kizazi.


“Jana tulikuwa tukiendelea na shughuli zetu za kutoa huduma za kibingwa na bingwa bobezi tulimpokea mgonjwa mwenye umri wa miaka 49 mwanamke ambaye amekua akiteseka na uvimbe kwenye kizazi kwa muda wa miaka 10 sasa", amesema Dkt. Ngadaya 


“Mara baada ya uchunguzi  tukagundua kuwa amekuwa  na hali ya uvimbe tumboni uliomsababishia kutofanya shuguli zake za kila siku za kujiingizia kipato”ameeleza 


Ameongeza kuwa  kwa kushirikiana na madaktari wa Hospitali ya Mangaka iliyopo  Halmashauri ya Nanyumbu ambapo madaktari bingwa wameweka kambi hiyo katika Masasi  waligundua kuwa uvimbe wake unahitaji kufanyiwa upasuaji.


Aidha amesema  kuwa ule uvimbe uliotolea wanafanya utaratibu wa kuusafirisha kwenda Hospitali ya Taifa  Muhimbili kwa vipimo na uchunguzi zaidi


Akizungumza mara baada ya upasuaji huo mgonjwa ambaye  jina lake  limeifadhiwa amesema anamshukuru Rais  wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kujali  wananchi  wake  na kuwasogezea  huduma za ubingwa na ubingwa bobezi karibu  kwani  hakuwa  na uwezo  wa kusafiri  na gharama  za kufanya upasuaji  huo.


“Leo najisikia vizuri hata hamu ya kula nimepata awali kabla ya upasuaji nilikuwa hata hamu ya kula sina namshukuru sana mama Samia kwa hii kampeni yake ya huduma za madaktari  bingwa bobezi ambayo imesaidia kuondolewa uvimbe ambao umenitesa kwa muda wote huo na kuninyima muda wa kufanya kazi za kuniingizia kipato”ameeleza