Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

DKT. JINGU AAGIZA KUUNDWA KAMATI MAALUM KUTATUA CHANGAMOTO ZA VIWANDA VYA NDANI VYA DAWA NA VIFAA TIBA

Posted on: May 24th, 2024



Na. WAF - Dar es Salaam

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu ameelekeza Waatalamu wa Wizara kushirikina na Chama cha wazalishaji wa Dawa nchini kuunda Kamati ya wataalamu itakayoshughulikia changamoto ili kuvilinda, kuboresha na kuvilea viwanda vya ndani vinavyotengeneza bidhaa za dawa

Dkt. Jingu ameyasema hayo Leo Mei 24, 2024 Jijini Dar Es Salaam wakati wa kikao kazi na wamiliki wa viwanda vya ndani vinavyotengeneza bidhaa za dawa nchini chenye la kujadili namna bora ya kuboresha mazingira ya uzalishaji wa Dawa nchini, ambacho kimekutanisha Viongozi kutoka MSD, TMDA, TANESCO, TRA, Wawakilishi kutoka Wizara ya Viwandana Biashara, Wizara ya Fedha, Wawakilishi kutoka Chama cha wazalishaji wa Dawa nchini,

Dkt. Jingu ametoa agizo hilo na kumkabidhi Mfamasia Mkuu wa Serikali Daniel Msasi kuhakikisha timu hiyo inapatikana na inakaa hadi kufikia Jumatano iweze kuja na mapendekezo ya nini kifanyike ili kuviendeleza viwanda vya ndani vya dawa na Vifaa Tiba.

"Sisi kama Serikali tunathamini Mchango wa Viwanda vya ndani vya Dawa vya binafsi sana lakini tunajua pia kuna changamoto na kwasababu ya izo changamoto ndio maana tumekutana, tuandae Mpango kazi ambao utaendana na hiki tunachokizungumzia leo na pia tupate kamati ya wataalamu watakao saidia kuchakata maoni yenu"

Katibu Mkuu pia amesisitiza juu ya matumizi sahihi ya kanuni na mara timu itakapopatikana ianze kazi mara moja ili Jumatano iweze kutoa Mrejesho wa hoja mbalimbali zinazowasilishwa na Wamiliki wa viwanda vya ndani vya dawa

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ameshauri kuwepo kwa mpango kazi utakaongoza serikali na wamiliki wa viwanda vya ndani vya dawa baada ya kuunda kamati ya wataalamu watakaosaidia kusimamia mipango ya muda mfupi na ile ya Muda Mrefu itakayochakata .

"Mimi pia nashauri tutengeneze timu itakayokuwa inachakata maoni ya wamiliki wa viwanda vya ndani vya dawa na Vifaa Tiba, pia tuwe na mpango kazi na tukubaliane tuwe na mikutano ya mara kwa mara ili sasa kuwe na muendelezo wa hivi vitu " amesema Prof. Nagu.