Wizara Ya Afya

SERIKALI YATOA MAELEKEZO 11 YA KUIMARISHA UTEKELEZAJI WA MPANGO JUMUISHI WA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII

Posted on: November 4th, 2026

Na Atley Kuni, WAF-Dodoma

Mkurugenzi Msaidizi Sehemu Epidemilojia Dkt. Vida Mmbaga kwaniaba ya Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Bruno Senguya ameita Mikoa na Halmashauri kuimarisha utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (iCCHW).

Maagizo hayo yametolewa wakati wa kikao kazi kilichofanyika Novemba 4, 2026, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mtumba.

Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Dkt. Mmbaga amesisitiza kuwa, Mpango wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ni uamuzi wa Serikali na si mradi, hivyo hakuna kurudi nyuma katika utekelezaji wake huku akiipongeza mikoa 12 na halmashauri 25 za awamu ya kwanza kwa kufanikisha mafunzo ya wahudumu 9,570 ambao tayari wamepewa mikataba na kuanza kutoa huduma.

Amezitaka Halmashauri kuhakikisha wahudumu wote waliofundishwa wanakamilisha mikataba ya kidigitali ndani ya siku 14, pamoja na kuhakikisha wanalipwa posho ya shilingi 100,000 kila mwezi kwa wakati na kusisitiza matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa na kuwasilishwa kwa taarifa za matumizi ndani ya siku 30.

Vilevile, amezitaka Halmashauri kujumuisha Mpango wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii katika mipango na bajeti za mwaka ujao wa fedha, kuimarisha usimamizi wa wahudumu, kutunza nyaraka zao kikamilifu na kuhakikisha vitendea kazi vinatunzwa na kutumika ipasavyo sambamb na huduma zote kuripotiwe kupitia mfumo wa UCS.

Kwa upande wa OWM-TAMISEMI, ameelekeza kuimarisha usimamizi wa utekelezaji kupitia Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri, kuweka viashiria vya Mpango katika tathmini ya utendaji wa Halmashauri na kuhakikisha maelekezo ya kikao yanawafikia Wakurugenzi Watendaji wote ndani ya siku saba toka tarehe ya kikao chao huku wataalam wa Wizara ya Afya wakielekezwa kufanya mapitio ya kati ya Mpango, kukamilisha Mkakati wa Uhamasishaji na Utafutaji wa Rasilimali pamoja na kuandaa Kadi ya Alama (Scorecard) ya kupima utekelezaji.

Amezitaka Halmashauri 159 ambazo bado hazijaanza utekelezaji kuanza maandalizi ya awamu inayofuata kwa kubaini vijiji na mitaa isiyokuwa na wahudumu, kuthibitisha mahitaji ya wahudumu wawili