Customer Feedback Centre

Ministry of Health

ZAIDI YA ASILIMIA 97 ZA RUFAA NCHINI WANAKWENDA INDIA

Posted on: October 28th, 2023


Na. WAF - Dar es Salaam


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa Tanzania na India imekuwa washirika wakubwa katika Sekta ya Afya ambapo zaidi ya asilimia 97 za Rufaa wanakwenda nchini India.


Waziri Ummy amesema hayo usiku wa leo Oktoba 28, 2023 wakati wa uzinduzi wa ofisi ya uratibu Hospitali ya Kokilaben Dhirubhai Ambani iliyoyopo Jijini Dar es Salaam. 


Aidha, Waziri Ummy amesema, Tanzania na India imekuwa washirika wakubwa katika Sekta ya Afya ambapo India imeweza kutoa mafunzo kwa maelfu ya kliniki nchini kwa wafanyikazi wa nyanja za usaidizi kama vile ushirika wa kimatibabu.


“Ushirika wetu umekuwa mkubwa sana katika Sekta ya Afya na sasa Tanzania inaagiza zaidi ya asilimia 80 ya bidhaa za dawa kutoka nje ya nchi ambapo asilimia 60 kati yake zinatoka India pekee”. Amesema Waziri Ummy 


Pia, amesema Taasisi za Afya za India zimeiongoza Tanzania katika kuanzisha programu maalum za kliniki nchini zikiwemo za upandikizwaji wa Figo, Upasuaji wa Moyo, Kupandikiza Mifupa (Uboho) pamoja na uwekaji wa Cochlear.


“Vilevile, Serikali ya Tanzania imewekeza pakubwa katika kubadilisha huduma za Afya kuelekea uangalizi maalum na wenye utaalam wa hali ya juu ili kuendelea kuboresha huduma za Afya zinazotolewa nchini”. Amesema Waziri Ummy 


Mwisho, Waziri Ummy amesema kuwa Tanzania imefanya uwekezaji mkubwa katika Miundombinu ya Huduma za Afya, Rasilimali Watu, mafunzo ya wataalam pamoja na wataalamu wa juu, kutokana na hali hiyo, Tanzania inatarajia kujibadilisha na kuwa kitovu cha utalii wa kimatibabu katika ukanda wa Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika.