Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WAZIRI UMMY AMSHUKURU RAIS DKT. SAMIA KWA KUSAINI SHERIA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Posted on: December 5th, 2023

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaini Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote.

“Shukrani sana Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujali Afya za wananchi wako husasani wa kipato cha chini na kukubali kusaini muswada wa sheria ya bima ya Afya kwa wote na sasa kuwa sheria kamili.” Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy Mwalimu amesema kazi iliyombele kwa sasa ni kuhakikisha utekelezaji wa Sheria hiyo inafanyika kwa ufanisi na kwa manufaa ya Watanzania hususani wa kipato cha chini ili kuwawezesha kupata huduma bora za Afya bila ya kikwazo cha pesa.

Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote ulipitishwa rasmi na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Spika Dkt. Tulia Akson Novemba Mosi, 2023 na kusaini na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Disemba 4, 2023 ili kuwa Sheria.