Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WAZIRI MCHENGERWA AWAPA KAZI WAKUNGA, WAUGUZI

Posted on: March 20th, 2024


*Awataka kuimarisha huduma, Mawasiliano

Na WAF - Dodoma


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikai za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka watumishi Wakunga na Uuguzi kusimamia utoaji wa huduma staha za afya zinazozingatia misingi ya huduma bora kwa mgonjwa.


Mchengerwa pia amehimiza mawasiliano madhubuti ili kwenda sambamba na uwekezaji uliofanywa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika sekta ya Afya.

Wito huo umetolewa kwaniaba yake na Mkurugenzi wa Afya na Ustawi wa Jamii wa Ofisi hiyo Dkt. Rashidi Mfaume Machi 20, 2024 wakati wa akifunga kikao kazi cha siku tatu cha kufanya tathimini ya utekelezaji wa huduma za uuguzi na ukunga jijini Dodoma.

“Ninawaelekeza mkasimamie wauguzi na wakunga wawe na lugha zenye staha na kufuata miongozo kwa wagonjwa ili wanachi wapate huduma bora hususani kipindi hiki ambacho Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mhe. Rais wetu mpendwa mama Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa kwenye miundombinu na vifaa tiba katika sekta ya Afya nchini.” Amesema.

Dkt. Mfaume amesema Serikali inatambua na kuthamini kazi na mchango mkubwa unaotolewa na Wauguzi na Wakunga nchini 


Kwa upande mwingine Dkt. Maumee amesema kuwa kada hizo źinawanawakilisha taswira kubwa ya sekta ya afya hivyo waendelee kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kutoa huduma bora kwa watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Uuguzi na Ukunga Wizara ya Afya Bi. Ziada Sellah akitoa salama za Wizara amewataka viongozi wauguzi na wakunga kutekeleza majukumu yao kwakuweka viashiria vya kujipima utendaji kazi wao na wanaowaongoza.

AidhabBi. Ziada amewataka wataalama hao kujiendeleza kielimu kwa kuchangamkia fursa za ufadhili unaotolewa na serikali kupitia Wizara ya afya lakini pia kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kujifunza ili kuongeza mbinu na ubunifu wa utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

MWISHO.