Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WANANCHI ZAIDI YA 2,700 TANGA WAPATA HUDUMA ZA UPIMAJI, USHAURI NA TIBA BILA MALIPO

Posted on: August 23rd, 2023

Na. WAF, Tanga

Wananchi zaidi ya 2,700 Mkoani Tanga na maeneo ya jirani wanufaika na kambi ya afya cheki kwa kupatiwa Huduma ya upimaji, ushauri wa afya na matibabu bila malipo ikiwa ni siku ya tatu katika kambi hiyo itakayodumu kwa muda wa siku tano mkoani humo

Kambi hiyo ikiwaimebakiza siku mbili kuisha bado wananchi wanaendelea kujitokeza kupata huduma mbalimbali za afya ambapo hadi sasa jumla ya watu 235 wamepata huduma za matibabu na dawa baada ya kuhisiwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB) kuanzia siku ya kwanza.

Aidha jumla ya waliopata huduma za uchunguzi wa macho ni takribani 805, na wote wamekutwa na changamoto na kupatiwa ushauri, tiba pamoja na dawa.

Huduma za Saratani ya Matiti na Mlango wa kizazi, jumla ya waliopata huduma ni 167, wenye tatizo la mlango wa kizazi ni Watano, wenye mabadiliko ya awali Saba, walipewa matibabu ya Tiba Mgando (cryotherapy) Wanne na waliopewa Rufaa ni Wawili.

Vile vile, huduma za upimaji wa ugonjwa wa Moyo zilikuwepo ambapo hadi leo jumla ya watu 102 wameshapata huduma hiyo, na watu 42 wamekutwa na tatizo la moyo na wote wamepata ushauri na matibabu pamoja na dawa.

Huduma za ugawaji wa dawa zilikuwepo kwa ambao walikutwa na tatizo ambapo hadi kufika leo siku ya Tatu kwenye kambi hiyo jumla ya wagonjwa 1,384 wamepatiwa dawa.

Upimaji wa UKIMWI, huduma hiyo nayo ilikuwepo na idadi ya wanaojitokeza kila siku ni kati ya watu 70 hadi 90 kupata huduma hiyo ya vipimo.

Elimu kinga dhidi ya madawa ya kulevya, waliohudhuria kupata huduma hiyo jumla ya watu 105 na ambao wanatumia ni watu 22 na wanatarajia kuacha matumizi hayo ya dawa za kulevya.

Ikumbukwe kuwa zoezi hilo la upimaji wa huduma za Afya bila malipo limeratibiwa na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. @ummymwalimu pamoja na Afya Cheki chini ya Mratibu wa mazoezi ya upimaji wa Afya bure (Afya Cheki) Dkt. Isack Maro kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga.