Customer Feedback Centre

Ministry of Health

WANANCHI WAKUMBUSHWA KUBADILI MTINDO WA MAISHA ILI KUKABILIANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA- PROF. MAKUBI

Posted on: December 9th, 2022

Na.WAF- Dodoma.

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Magonjwa Yasiyoambukiza kwa kubadili mtindo wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi, kuepuka matumizi ya pombe kupita kiasi, kuacha uvutaji bidhaa za tumbaku na kula lishe bora wakati wote.

Prof. Makubi amesema hayo leo wakati akiongoza Watumishi wa afya kufanya mazoezi katika mji wa Serikali Mtumba ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kupambana dhidi ya Magonjwa Yasiyoambukiza katika miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania yenye kauli mbiu ya "Amani na Umoja ni nguzo ya Maendeleo yetu."

Amesema, Magonjwa Yasiyoambukiza, Afya ya Akili na Ajali ni changamoto kubwa kwa sasa katika jamii yetu, hivyo wito wangu kwa Viongozi na wananchi wote kuelimishana juu ya mtindo bora wa maisha ili kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo kufanya mazoezi, kuacha au kupunguza matumizi ya vileo pamoja na kula lishe bora.

" Magonjwa Yasiyoambukiza , Afya ya Akili na Ajali ni changamoto kubwa kwa sasa katika jamii yetu. Tunatoa wito kwa Viongozi na wananchi wote kuelimishana juu ya kinga ,kufanya mazoezi pamoja na kula lishe bora." Amesema Prof. Abel Makubi.

Aidha, ametoa wito kwa Wananchi na Wataalamu kuendelea kuelimishana ili kujiunga na Bima ya afya kwa wote pindi Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote utakapopitishwa, jambo litalosaidia wananchi kupunguza gharama za matibabu na kupata huduma kwa kituo chochote kuanzia ngazi ya Zahanati hadi hospitali ya Taifa.

Sambamba na hilo Prof. Makubi akiongozana na Watumishi wa Wizara ya Afya na Taasisi zake ametembelea ujenzi wa mradi wa ofisi za Wizara ya Afya katika mji wa Serikali Mtumba ili kujionea maendeleo ya mradi huo ambao umefika 40% mpaka kukamilika kwake.

Katika ukaguzi huo Prof. Makubi amewaelekeza Wakandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ulio nyuma kwa 10% kulingana na makubaliano ili mradi huo uanze kutumika.

Sambamba na hilo amewaelekeza Mkurugenzi wa Utawala na Mkuu wa Kitengo cha ujenzi kutembelea mradi huo kila wiki na kutoa taarifa ya maendeleo ya mradi huo...