Customer Feedback Centre

Ministry of Health

UELEWA MDOGO CHANZO CHA UTAPIA MLO KWA JAMII

Posted on: July 23rd, 2024


 

Na. WAF – Dar Es Salaam.

 

Uelewa mdogo wa jamii kuhusu masuala ya lishe ikiwemo matumizi sahihi ya vyakula vinavyopatikana katika maeneo mbalimbali ya nchi ni miongoni mwa sababu zitajwa kuchangamoto utapiamlo ndani ya jamii.

 

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma Lishe Wizara ya Afya Bi. Neema Joshua Julai 23, 2024 jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na Viongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania, ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kuhakiki na kupitisha maudhui ya jumbe zilizopo kwenye rasimu ya mwongozo wa viongozi wa dini wa uhamasishaji na uelimishaji jamii juu ya masuala ya lishe nchini.

 

Bi. Neema amesema ili kuondoa changamoto ya utapiamlo kwa nchi Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea kushirikiana na Viongozi wa dini ili kuhakikisha elimu na uhamasishaji wa lishe bora unawafikia watanzania waliowengi.

 

“Lishe bora ni msingi wa ustawi mzima wa maisha ya binadamu katika nyanja zote za Maisha, nidhahiri kuwa, afya njema ambayo kwa kiasi kikubwa huchagiwa na Lishe bora, humwezesha mtu kutimiza majukumu yake ya kila siku kwa ufanisi ikiwemo kushiriki katika ibada, sala, kutafakari pamoja na kufanya kazi kwa tija kwa maendeleo yake binafsi, jamii na Taifa kwa ujumla" amesema Neema na kuongeza

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Jimbo kuu la Kusini mwa Tanzania, Mchungaji Dkt. Jeremiah Izungo amesema ameishukuru Wizara ya Afya kwa maono yake ya kuona umuhimu wa Viongozi wa dini kushirikishwa kwenye masuala ya lishe jambo ambalo linawapa nguvu ya ziada viongozi wa dini kulisemea kwa waumini wao.

 

Katika hatua nyingine amesema mwili wa binadamu ni hekalu la mungu na ni mali yake hivyo changuo ya namna ya kula na nini chakula ni lazima kizingatia mratibu wa mwili ambae ni Mungu, kufanya vinginevyo ni kumkosea na kukatisha maisha ya mwanadamu.

 

“Ili tuwe salama tunapaswa kuupende huu mwili sawa sawa na mapenzi ya mwenye mwili na sio vinginevyo¹, “Basi mlapo au mnywapo au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa mungu”; 1 Wakorintho 10;31” amesema Mch. Dkt. Izungo