Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TMDA WAPEWA JUKUMU LA USIMAMIZI WA MADUKA YA DAWA

Posted on: November 9th, 2023


-Ongezeko la matumizi holela ya Dawa za Antibiotiki


Na. WAF - Dodoma


Usugu wa vimelea dhidi ya dawa mwilini (Antimicrobial resistance AMR) ni tishio kubwa la afya kwa jamii ya Watanzania hivyo Serikali imeweka mikakati madhubuti ili kukabiliana na tatizo hilo kwa kuimarisha udhibiti kwa kuondoa usimamizi wa maduka ya Dawa kutoka Baraza la Famasi na kupeleka majukumu haya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)


Waziri Ummy amebainisha hayo kwenye ukurasa wake wa mtandao X wakati akijibu hoja ya Frank Arabi alipohoji kuhusu matumizi sahihi ya dawa za antibiotiki.


Waziri Ummy amesema kumekuwepo na matumizi yasiyo sahihi ya dawa nchini na hivyo kufanya dawa nyingi za Antibiotiki hivyo kuwa na ufanisi mdogo katika kutibu magonjwa.  


“Pamoja na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya dawa za Antibiotiki, tatizo hii kwa kiasi kikubwa linachochewa na baadhi ya wataalam wetu kwenda kinyume na kanuni na miongozo ya taaluma”. Amesema Waziri Ummy.


Waziri Ummy amewataka wahudumu wa Afya hasa Madaktari na Wafamasia kusimamia jukumu hilo ili Watanzania wapate uelewa juu ya matumizi sahihi ya dawa.