Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TANZANIA MFANO MAPAMBANO YA KUPNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI.

Posted on: February 14th, 2024



Na WAF - Dodoma

Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani JICA limeitaja Tanzania kama mfano wa kuigwa kwa nchi za Afrika na Duniani kwa ujumla katika mapambano ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa kuwa inafanya vizuri kulinganisha na nchi nyingine.

Hayo yamebainika wakati wa uwasilishaji wa mradi kutoka Shirika la ushirikiano wa kimataifa la Japan (JICA) wenye lengo la kufanya uboreshaji wa huduma za mama na mtoto mchanga uliokuwa ukiwasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. John Jingu Leo Februari 14, 2024, Jijini Dodoma.

Mara baada kupoke wasilisho hilo Dkt. Jingu amesema uwepo wa matokeo chanya katika utekelezaji wa mipango na mikakati mbalimbali nchini ndio umekuwa ukihamasisha zaidi wadau kuzidi kuwezesha Miradi zaidi ya kuboresha huduma za afya nchini hasa masuala ya mama na mtoto.

"Tunalishukuru Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japani JICA na Nchi ya Japan kwa misaada inayotoa kwa Tanzania. utekelezaji wa miradi hii utasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini. Na sisi tunaahidi kutoa ushirikiano utakaohitajika katika utekelezaji wa miradi hii." Amesema Dkt. Jingu

Kwa upande wake Mshauri Mkuu, Idara ya Utafiti na Mipango Bw. Kiyomasa Machida amesema Mradi huo unalenga kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto kwa kuimarisha mifumo ya uchunguzi na matibabu ya kikanda kwa kutoa vifaa tiba vinavyohusiana na afya ya mama na mtoto kwa Hospitali za rufaa za mikoa saba (7) Tanzania Bara na Zanzibar/Unguja.

"Hospitali zinazotazamiwa ni Dodoma RRH, Katavi RRH, Ligula RRH, Mount Meru RRH, Sekou Toure RRH, Tumbi RRH, Lumumba RH katika ya Sehemu Ununuzi wa Vifaa vya Matibabu Vifaa vinaweza kutumika kwa huduma za matibabu, utambuzi, matibabu, haswa utunzaji wa mama na mtoto mchanga." amesema Machida