Customer Feedback Centre

Ministry of Health

TANZANIA, GLOBAL FUND KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA AFYA

Posted on: February 8th, 2025

Na WAF, USWISI

Naibu Katibu Mkuu Bw. Ismail Rumatila na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe Februari 6, 2025, wamekutana na Dkt. Linden Morrison wa Mfuko wa Dunia (Global Fund) jijini Geneva, Uswisi, kujadili mikakati ya kuboresha huduma za afya nchini.

Katika mazungumzo hayo, Tanzania imeeleza hatua inazoendelea kuchukua ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za Kifua Kikuu, UKIMWI na Malaria ikiwa ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa dawa na bidhaa muhimu za kutibu magonjwa hayo.

Kwa upande wao Global Fund imeeleza kuwa uhusiano wake na Tanzania umekuwa wa muda mrefu na umechangia kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma za afya nchini.

Aidha, Global Fund imeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania ili kuimarisha zaidi sekta ya Afya.