Customer Feedback Centre

Ministry of Health

SERIKALI YAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA NGAZI ZOTE

Posted on: August 16th, 2025

Na WAF, Dodoma

Serikali imeendelea kuimarisha huduma za afya ikiwepo miundombinu ya kutolea huduma, upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa, huduma za mama na mtoto, ongezeko la ujuzi, Ubingwa bobezi na huduma za Kibingwa kwa Hospitali za Rufaa za Mikoa na ngazi ya Msingi
 
Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa Agosti 15, 2025, mbele waandishi wa habari mkoani Dodoma, Uboreshaji hadi sasa umetumia fedha kiasi cha shilingi Trilion 8.9 ndani ya kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita.

"Katika Kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, vituo vya kutolea huduma za afya vimeongezeka kutoka 10,153 mwaka 2021 hadi vituo 12,846 Aprili 2025, Idadi hii inajumuisha pia kliniki za magonjwa maalum na maabara binafsi" amesema Msigwa na kuongeza

“Serikali ya Awamu ya Sita (6) imeendelea na maboresho ya miundombinu ya kutolea huduma za afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa majengo mapya, ukarabati na ukamilishaji wa majengo katika hospitali mpya kwenye mikoa mipya mitano. Maboresho hayo yamegharimu jumla ya shilingi za kitanzania Trilioni 1.04 na yalifanyika katika maeneo yafuatayo,” amesisitiza Msigwa.

Katika hatua nyingime Msingwa amesema, Serikali imeendelea kushirikiana na sekta binafsi ili kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya nchini.
 
“Zahanati binafisi zimeongezeka kutoka 2,106 mwaka 2020 hadi kufikia 2,272 Aprili, 2025, Vituo vya afya binafsi vimeongezeka kutoka 323 mwaka 2020 hadi kufikia 349 Aprili 2025 na,Hospitali binafsi zimeongezeka kutoka 173 mwaka 2020 hadi kufikia 212 Aprili, 2025 zikiwa katika hadhi mbalimbali kuanzia ngazi ya Wilaya, Mkoa hadi Kanda,” amesema Bw. Msigwa.

Mbali na uboreshaji huo Msemaji huyo Mkuu wa Serikali amefafanua kuwa, Serikali imefanikiwa kuanza utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote namba 161 kwa kukamilisha maandalizi ya Kanuni za Bima ya Afya kwa Wote Hatua ambayo inawezesha Serikali kuanza utekelezaji wa awali wa Bima ya Afya kwa wote sambamba na utaoaji elimu kwa wananchi na viongozi wa ngazi zote.

“Katika kipindi cha kuanzia Julai, 2024 hadi Mei, 2025 kiasi cha Shilingi Bilioni 166.52 kimekusanywa. Ku