Customer Feedback Centre

Ministry of Health

RAIS DKT. SAMIA ATEKELEZA KWA VITENDO AZMA YAKE KWA KILA MTANZANIA KUPATA HUDUMA BORA ZA AFYA

Posted on: February 10th, 2025

Na WAF - SINGIDA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani amezidi kuhakikishia umma na wakazi wa Mkoa wa Singida na maeneo ya jirani adhma yake ya kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za Afya baaada kufufua na kuendeleza Mradi wa Ujenzi wa jengo la hospitali ya Mkoa Singida ulioanza tangu 2014.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Singida Dkt. David Mwasota amebainishwa hayo jana Februari 7, 2025 katika taarifa yake aliyoitoa mbele ya timu ya wataalamu toka Wizara ya Afya ambao walikua wakiendesha zoezi la usimamizi shirikishi katika Hospitali hiyo.

Taarifa imebainisha kuwa licha ya ujezi wa mradi huo ulianza 2014 ujenzi ulisimama kwa takribani miaka 6 (2014 - 2020), na kuendelea kidogo mwaka 2020 na baadae Serikali ya awamu ya Sita kuendeleza kazi hiyo hadi sasa ujenzi huo upo 78% kwa sakafu ya chini na asilimia 36% kwa sakafu ya pili huku kiasi kilichotumika kwenye ujenzi hadi sasa ni zaidi ya Tsh.3bil za kitanzania.

Kukamilika kwa mradi huo kunaenda kuboresha huduma za Wodi ya magonjwa ya wanawake Wodi za kulaza watoto ambapo kwa sasa wanatumia Ofisi za Jengo la Utawala kama wodi, Wodi za upasuaji na Wodi za kulaza Wagonjwa kwa Magonjwa ya ndani.

Taarifa imeongeza kuwa kukamilika kwa mradi kutatanua wigo wa huduma za Wodi za kulaza Wagonjwa wa Upasuaji Huduma za uangalizi maalum kwa wagonjwa, Wodi za kulaza viongozi, Huduma za uchunguzi mfumo wa chakula Vyumba vya upasuaji sambamba na Huduma za Maabara, Famasi, utengamao na utasihishaji vifaa.

Taarifa ya Dkt. Mwasota pia amebainisha miradi mingine ya ujenzi inayoendelea ni pamoja na Ujenzi wa jengo la “Medical Oxygen Plant” chini ya ufadhili wa Global Fund ambapo mradi unaendelea na unatarajiwa kugharimu kiasi cha Tsh. Mil. 262, na unatarajiwa kukamilika mwezi Machi 2025.

Aidha, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Singida imekamilisha ujenzi wa Jengo la Huduma za dharura na Jengo la Huduma za wagonjwa Mahututi (ICU) yenye thamani ya Tsh.1 Bil. zikiwa ni fedha kutoka serikali kuu na sasa majengo yanatumika.