Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MPANGO WA MIAKA 5 WA UWEKEZAJI KATIKA AFYA YA MAMA NA MTOTO WAZINDULIWA

Posted on: August 23rd, 2023

Na WAF - ZANZIBAR

Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman amezindua Mpango wa Uwekezaji katika Afya ya Mama na Mtoto Tanzania wa miaka mitano (Tanzania Martenal & Child Health Investment Program) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Global Financing Facility wenye lengo la kuimarisha afya ya Mama na mtoto nchini.

Akizundua Mpango huo leo Agosti 23,2022 Zanzibar Mhe. Othman amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi kwa kuendelea kuipa kipaombele Sekta ya Afya na kuweza kuzindua mpango wa uwekezaji katika Afya ya mama na mtoto ambao unalenga kuboresha huduma za Afya ya Mama na Mtoto katika ngazi zote za utoaji wa huduma za afya nchini.

Amesema Mpango huo utatekelezwa chini ya Usimamizi wa Wizara ya Afya Tanzania Bara, Wizara ya Afya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI ambapo uwekezaji wake utagharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 275 ambapo kiasi cha dola za Marekani 250 ni mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Dunia na kiasi cha dola za Marekani milioni 25 kutoka Global financing facility.

Amesema kuwa kwa upande wa Tanzania Bara Mpango huu utatekeleza afua muhimu ikiwemo kuajiri watumishi 1000 wa kada mbalimbali za afya, kufanya ukarabari wa vituo 159 vya kutolea huduma za afya, ununuzi wa vifaa tiba kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya ya mama na mtoto, kuimarisha mfumo wa magonjwa ya dharura na rufaa kwa akina mama wajawazito na watoto wachanga pamoja na kuimarisha menejimenti na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya.

Huku, upande wa Zanzibar ni uimarishaji wa huduma za afya ya mama na mtoto na kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi

Mwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya Tanzania Bara Mhe Godwin Mollel amewataka Wataalamu kuhakikisha sehemu ya fedha hizi kuelekezwa kwenye eneo la lishe katika kipindi cha ujauzito na baada ya mama kujifungua ili kupata watoto wenye uwezo mkubwa kiakili na afya bora utaosaidia katika kuleta maendeleo nchi