Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MAJERUHI WA MAFURIKO YA HANANG WOTE WAMETIBIWA MANYARA BILA YA RUFAA.

Posted on: December 6th, 2023Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Tulia Ackson ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa uboreshaji wa huduma za afya nchini na kufanya majeruhi wote wa mafuriko ya Hanang kupata huduma Mkoani Manyara bila kupewa rufaa.

"Nampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuhudumia vyema majeruhi wa mafuriko na kutibiwa bure bila gharama yeyote" amesema Dkt. Tulia.

Aidha ameipongeza Wizara ya Afya na wataalamu wote kwa kazi nzuri waliofanya katika kuwahudumia majeruhi hao na kuwataka wataalam kuendelea kutoa huduma bora za matibabu kwa wananchi.