Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MADAKTARI BINGWA WA SAMIA, WAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI HOSPITALI YA WILAYA MAFIA

Posted on: June 6th, 2024


Na WAF- Mafia


Timu ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia wanaendelea kufanya zoezi la kuwajengea uwezo watumishi katika Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Mafya sambamba na kutoa huduma wilayani humo.



Madaktari hao walioweka kambi visiwani humo licha ya kutoa huduma kwa wananchi zoezi lingine limekuwa kuwajengea uwezo watumishi wa eneo husika ili wapate uzoefu wa utoaji huduma bora kwa wananchi.


Kingozi wa Madaktari Bingwa walioweka kambi ya siku tano katika Hospitali ya Wilaya ya Mafia Dkt. Mwasamila amesema zoezi hilo ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za afya katika maeneo ya vijijini na visiwani.


"Kazi ambayo inafanyika inajumuisha kutoa mafunzo ya kitaalamu, kuboresha ujuzi na maarifa ya watumishi wa afya, na kuhakikisha kuwa huduma bora za afya zinapatikana kwa jamii zote. Amesema Dkt. Mwasamila.


Pia Dkt Mwasamila amesema Jitihada hizo ni sehemu ya mpango wa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuboresha sekta ya afya nchini, hasa katika maeneo ya pembezoni na visiwani ambavyo huduma za afya zimeqalia kuwa duni.


Aidha, kwa upande wa Uongozi wa Hospitali hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia ambae pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya wanawake na Uzazi Dkt. Said Issa Maya amesema, Madaktari hawa bingwa wameweza kutoa mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafia.


Ujio wa madaktari Bingwa kwa siku tano kwenye Hospitali ya wilaya ya Mafia wamewezesha kuboresha vifaa na teknolojia inayotumika hospitalini hapo.


Mwisho