Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MADAKTARI BINGWA WA SAMIA WATUA NJOMBE, WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA

Posted on: October 28th, 2024

Na WAF – Njombe

Wananchi wa Mkoa wa Njombe wametakiwa kutumia fursa ya uwepo wa madaktari bingwa na bobezi katika hospitali za halmashauri zote sita ili kupata matibabu ya kibingwa.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Bi. Judica Omari, alipo mwakilisha Mkuu wa mkoa huo... jina la Mkuu wa Mkoa).. huku akikutoa wito kwa wananchinkujitokeza kwa wingi ili kukutana na Mabingwa hao.

"Katika awamu ya kwanza, wananchi wengi wamehudumiwa na mafanikio yamekuwa makubwa, sasa tupo katika awamu ya tatu, na huduma hizi za kibingwa zimesogezwa karibu zaidi na wananchi wetu. Nawasihi mjitokeze kwa wingi katika hospitali za halmashauri ili kupata huduma hizi zenye kiwango cha juu," amesema Bi. Judica.

Bi. Judica ameongeza kuwa anatoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuwapatia wananchi huduma za kibingwa karibu na kupunguza gharama za kusafiri.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dkt. Juma Mfanga, amesema kuwa madaktari hao wamekuja kwa muda mfupi na wanatarajiwa kuwajengea uwezo watumishi wa afya kwenye hospitali hizo, jambo ambalo litaimarisha huduma kwa wananchi.

“Tunawaomba wananchi wafike hospitalini ili kupata huduma hizi za kibingwa. Fursa hii ni adimu, na madaktari hawa wanakuja mara chache, hivyo ni muhimu kuitumia vizuri,” amesisitiza Dkt. Mfanga.

Naye Mratibu wa Kambi ya Madaktari Bingwa wa Samia kutoka Wizara ya Afya, Bi. Cephlene Budodi, amesema lengo kuu la kambi hiyo ni kusogeza huduma za kibingwa na kupunguza gharama za kufuata huduma hizo mbali.

Ameeleza kuwa serikali imeendelea kuimarisha huduma za afya, ikiwemo kuanzisha wodi maalum kwa watoto wachanga wagonjwa na waliozaliwa na uzito pungufu (NCU).

Madakari Bingwa wa Rais Samia wapo kwenye mikoa ya Ruvuma, Iringa na Njombe kwenye Halmashauri zote za mikoa hudika na watatoa huduma hadi Novemba 02, 2024