Customer Feedback Centre

Ministry of Health

MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA WAIMARISHA MATIBABU YA MOYO MKOANI SHINYANGA.

Posted on: June 19th, 2024


Na WAF - SHINYANGA


Uwepo wa Kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia Mkoani Shinyanga wenye lengo la kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi hasa ngazi ya afya ya Msingi, umeimarisha upatikanaji wa Huduma za kiuchunguzi na matibabu ya Moyo katika Hospitali ya Wilaya ya Dr. Jakaya Mrisho Kikwete iliyopo wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga


Hilo limebainishwa Juni 19, 2024 Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, na baadhi ya wanufaika wa huduma hizo ambapo wamesema Huduma za kibingwa wanazoendelea kusogezewa na kupatiwa zitasaidia kupunguza gharama walizokuwa wakitumia kufuata huduma za Matibabu ya moyo katika hospitali za mbali hasa Muhimbili KCMC na Bugando.


Akizungumza manufaa yaliyopatikana kutokana na kambi hiyo Bi. Suzana Hezron Isaya Mkazi wa wilaya ya Kishapu amefurahishwa na Ujio wa madaktari bingwa wa moyo ambapo ilimpasa kusafiri umbali mrefu ili kufata huduma hiyo na kuipongeza Wizara ya Afya kwa kutii agizo la Mh. Rais Samia Suluhu Hassan la kupeleka madaktari bingwa katika wilaya hiyo.


“Mimi nawashukuru Wizara ya Afya kwa kutii maagizo ya mama, Mama anaposema fanya hivi mnaitika” amesema Bi. Anna Hezron


Bw. Pankras Maganga pia ni miongoni mwa wanaufaika wa Huduma za kibingwa amesema ameishukuru Serikali kwa kushusha huduma kwa wananchi na kuomba elimu iendelee kutolewa ili wananchi waweze kufika kupata huduma za kibingwa.


Nae Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga Dr. Elieth Mchuruza amesema kuwa uwezo ambao wataalamu wa kituo chake wamejengewa na Madaktari Bingwa utatumika katika kuongeza ubora wa utowaji huduma kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.