LITA 10,000 ZA HEWA TIBA YA OKSIJENI KUZALISHWA KILA SIKU KATIKA HOSPITALI YA MUSOMA DC
Posted on: July 2nd, 2024
Hospitali ya Wilaya ya Musoma Vijijini, Mkoani Mara iko mbioni kuanza uzalishaji wa hewa tiba ya Oksijeni lita Elfu kumi (10,000) kwa siku jambo litakalosaidia wakazi wa wilaya hiyo, mkoa wa Mara na maeneo ya Jirani kuondokana na adha kwa wagonjwa wa dharula.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Eliyangilinga Moshi Julai Mosi, 2024 ambapo amesema uzalishaji huo unategemewa kuanza mapema mwezi Agosti 2024.
“Tutakapoanza tunatarajia kuzalisha mitungi mia mbili ambapo kila Mtungi mmoja utabeba lita 50 za gesi ya Oksijeni kwahiyo ukizidisha hapo jumla tutakuwa tunazalisha jumla ya lita zipatazo 10,000 kwa siku moja’’. Amesema Dkt. Moshi.
Dkt. Moshi ameongeza kuwa wanufaika wa hewa tiba hiyo kulingana na mahitaji ni wakazi wa wilaya Musoma vijijini ambao kwa muda mrefu iliwalazimu kuipata Musoma Mjini ili
“Mbali na wenyeji wa Musoma vijijini pia wakazi wote wa