Customer Feedback Centre

Ministry of Health

LISHE DUNI NI VITA YA PAMOJA

Posted on: July 24th, 2024



Na WAF - Dar Es Salaam


Serikali imesema suala la lishe duni chini ni vita yenye athari kubwa kwa taifa huku ikiwataka wadau na viongozi wa dini kuunganisha nguvu kukabiliana nayo.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za

Lishe Wizara ya Afya, Bi. Neema Jushua, Julai 24, 2024 jijini Dar Es Salaam wakati akizungumza na viongozi wa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ikiwa ni muendelezo

wa vikao kazi vya kuhakiki na kupitisha maudhui ya jumbe zilizomo kwenye rasimu ya mwongozo wa viongozi wa dini

wa uhamasishaji na elimishaji jamii kuhusu masuala ya lishe

nchini.


Bi. Neema amesema lishe ina uga mpana sana kwenye maendeleo ya taifa.


"Hali ya lishe ya nchi yetu imeharibika na lishe mbovu na hili linaweza kutishia usalama wa nchi kwa kuwa watu wake hawazingatii milo sahihi na mitindo bora ya maisha yao. Endapo watu hawana uwezo wa kufikiri sawa sawa kwa kujitengenezea wenyewe na kutegemea kutoka nje, hali hii

inaweza kuathiri usalama wa nchi."


Awali, akimkaribisha Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe kutoka Wizara ya Afya, Bw. Japhet Msoga amesema lengo la kikao hicho ni kupitisha maudhui ya ujumbe yaliyomo kwenye rasimu ya mongozo kwa ajili ya matumizi

na viongozi wa dini na kuwasilisha nadharia ya lishe kwa viongozi wa dini kwa ajili ya kujenga uelewa kuhusu masuala ya lishe.


"Lengo ni kuendeleza ushirikiano kati ya viongozi wa dini na Wizara ya Afya kwenye juhudi za kuboresha hali ya lishe nchini ambapo matarajio ya Wizara ya Afya ni kupata Mwongozo wa Viongozi wa Dini wa Uhamasishaji na Uelimishaji Jamii kuhusu masuala ya lishe nchini."