Customer Feedback Centre

Ministry of Health

HUDUMA ZA KIBINGWA KUSOGEZWA KARIBU ZAIDI KWA WANANCHI.

Posted on: December 18th, 2022

Na. WAF- Dodoma

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu ametoa wito kwa Hospitali za Taifa, kanda na Hospitali za Rufaa za mikoa kutoa huduma za kibingwa na bobezi kwa hospitali za Halmashauri kwa njia ya mkoba ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi

Prof. Nagu ametoa wito huo leo Jijini Dodoma wakati wa kufunga kikao kazi cha Menejimenti na Taasisi za Wizara ya Afya chenye lengo la kujadili utendaji kazi wa Wizara na Taasisi zake ili kuboresha Huduma za Afya nchini.

Ameendelea kwa kusisitiza kuwa, Waganga wakuu wa Halmashauri nchini watumie mapato ya ndani ya hospitali zao kuwezesha madaktari bingwa na bobezi kufika katika hospitali wilaya na kutoa huduma za kibingwa na bobezi kwa wananchi.

“Hakikisheni Sekta ya afya tunatembea pamoja ili kuimarisha utendaji kazi kwa kusimamia Sera na miongozo na kutoa huduma bora kwa wananchi." Amesema.

Aidha Prof. Nagu amewasisitiza Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Afya Pamoja na Waganga wakuu wa wilaya kutoa elimu ya musuada wa Bima ya afya kwa wote kwa wananchi ili kuwa na uelewa pamoja ikiwa ni kuelekea kupitishwa kwa muswada wa Bima ya Afya kwa wote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe , Ofisi ya Rais , Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. @ntulikapologwe amesema, kama watekelezaji wa Sera na miongozo wanakwenda kuratibu kwa kuweka ratiba ya kuhakikisha madaktari bingwa na bobezi wanafika katika hospitali za wilaya na wanatoa huduma bingwa na bobezi kwa wananchi.

“Na kwa kufanya hivi itasaidia kuimarisha mnyororo wa huduma za rufaa kuanzia ngazi za chini mpka ngazi ya taifa ambapo ili huduma tembezi itapunguza wananchi kusafiri umbali mrefu kufata huduma za kibingwa na bobezi.” ameeleza @ntulikapologwe

@ntulikapologwe amesema kwa kufanya vile watakuwa wanatumia vizuri kiasi cha shilingi Billion 95 zilizotolewa kwa ajili ya kununua vifaa tiba vya kisasa katika hospitali za wilaya nchini zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan