Customer Feedback Centre

Ministry of Health

ELIMU ITOLEWE KATIKA MCHAKATO WA KUPATA WAHUDUMU WA AFYA NGAZI YA JAMII.

Posted on: June 12th, 2024


Na WAF, NJombe.


Mhe. Anthony Mtaka Mkuu wa Mkoa wa Njombe ameongoza kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.


Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Makatibu Tawala wa Halmashauri zote za Mkoa wa Njombe, Waganga Wakuu wa Halmashauri na wajumbe wa kamati za uendeshaji wa shughuli za afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri (RHMT & CHMT).


Akiongea wakati wa kufunga kikao, Mhe. Anthony Mtaka aliishukuru Sekta ya Afya kwa jitihada zake za kuboresha huduma za afya hususani huduma za afya ngazi ya jamii. Pia alielekeza kuwa taarifa ya afya ya msingi iwe ni sehemu muhimu ya taarifa ya idara ya afya ngazi zote ikiwemo Mkoa na ioneshe matokeo Chanya ya mpango ili kujenga hoja za kutekelezwa katika Halmashauri zingine.


Na alihimiza Halmashauri kutumia mapato ya ndani kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwemo kuwakatia bima, Alielekeza matokeo chanya ya mpango yawekwe wazi kwa wananchi na jamii ijue kwani uwekezaji uliofanyika katika Mkoa wa Njombe katika kutekeleza mpango huu ni mkubwa akitolea mfano malipo ya kila mwezi ya CHW yatakayowanufaisha CHWs 746 na ni fursa ya ajira kwa wananchi wa Njombe.


Pia alihimiza wasimamizi na watekelezaji kuzingatia Miongozo iliyotolewa na Wizara.