Wizara Ya Afya

WAZIRI MCHENGERWA ATANGAZA MABALOZI WA BIMA YA AFYA KWA WOTE

Posted on: October 22nd, 2026

Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa, ametangaza mpango wa kuteua Mabalozi wa Bima ya Afya kwa Wote katika kila wilaya nchini kwa lengo la kuongeza uelewa wa wananchi na kuhamasisha usajili katika mpango huo unaolenga kupanua upatikanaji wa huduma za afya.

Waziri Mchengerwa, ametangaza mpango huo leo Oktoba 22, 2026, mkoani Mtwara wakati wa hafla ya kuanza rasmi kwa usajili wa Bima ya Afya kwa Wote Awamu ya Pili, akieleza kuwa ushiriki wa jamii ni muhimu ili kuhakikisha elimu kuhusu bima inawafikia wananchi katika maeneo wanayoishi na kufanya shughuli zao za kila siku.

"Mabalozi hao watatoka katika makundi mbalimbali, yakiwemo viongozi wa dini na kimila, walimu, wataalamu wa afya, wasanii, wanamichezo, wafanyabiashara, wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na viongozi wa wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu," amesema Mhe. Mchengerwa

Aidha, Mhe. Waziri Mchengerwa ameeleza kuwa mabalozi hao watakuwa na jukumu la kuelimisha na kuhamasisha wananchi kujiunga na bima, kwa kushirikiana na viongozi wa wilaya katika kufuatilia maendeleo ya usajili na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Amesema, utekelezaji wa mpango huo utaambatana na tathmini za mara kwa mara, ambapo mabalozi watakutana na Wakuu wa Wilaya kila mwezi kujadili maendeleo ya uandikishaji, huku taarifa zikiwasilishwa kwa Wizara kila robo mwaka ili kufuatilia matokeo ya juhudi hizo.

Pia, Waziri Mchengerwa amewahimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika kulinda uendelevu wa Bima ya Afya kwa Wote kwa kuepuka udanganyifu, ikiwemo kutumia kadi za watu wengine, kutoa taarifa za uongo au kuwasilisha madai ya huduma ambazo hazikutolewa kwa wagonjwa.

"Serikali itaendelea kuimarisha mifumo ya kidijitali na usimamizi wa kisheria kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) ili kuhakikisha watoa bima wanatimiza wajibu wao, madai yanashughulikiwa kwa haki na wanufaika wanapata huduma wanazostahili," amesema Mh. Waziri Mchengerwa

Akizungumzia umuhimu wa ushiriki wa wananchi, Mhe. Mchengerwa amesema awamu ya kwanza iliwezesha kusajili kaya 198,709 za wananchi wasio na uwezo, huku awamu ya pili ikile