Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

TANZANIA KUENDELEA KUTOA KIPAUMBELE MASUALA YA LISHE KWA NCHI WANACHAMA

Posted on: August 30th, 2023

Na WAF, Gaborone - Botswana


Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Agosti 30, 2023 ameendelea kushiriki kikao cha 73 cha Mawaziri wa Afya wa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika chenye lengo la kujadili masuala mbalimbali katika Sekta ya Afya.  


Tanzania ni miongoni mwa nchi wanachama wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika ambapo kupitia Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu imebainisha kuendelea kupambana na tatizo la upungufu wa chakula na lishe bora inayopelekea ukondefu (Malnutrition).


Mawaziri wa Afya wa Nchi wanachama wa WHO Kanda ya Afrika wakati wakiendelea kuchangia mada katika kikao hicho wamesema sababu zinazopelekea kupungua kwa uzalishaji wa chakula ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, changamoto zilizotokana na ugonjwa wa COVID-19, ukame na mafuriko.


Pia, wamesema nchi cha Afrika zimeonesha ongezeko la matatizo yatokanayo na ukosefu wa lishe ni pamoja na kutozingatia ulaji sahihi wa vyakula (Balanced diet). 


Kwa upande wa wadau pamoja na mashirika ya Kimataifa yanayojishughulisha na masuala ya chakula na lishe wakiwemo UNICEF, FAO, Sun MOVEMENT, AFRICAN UNION, Nutrition International na wengine wameahidi kuendelea kusaidia kuchangia na kushirikiana na Serikali za Afrika kwa lengo la kupunguza changamoto zitokanazo na lishe.