Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

RUFAA YA KWENDA BMH YAZUIWA NA MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA

Posted on: September 28th, 2024

Na WAF, Kiteto - Manyara

Madaktari Bingwa wa Rais Samia walioweka kambi katika hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Kiteto mkoani manyara wamefanikiwa kumfanyia upasuaji mwanaume mwenye umri wa miaka 50 aliyesumbuliwa na kukunjika kwa utumbo na kuzui rufaa aliyoandikiwa kwenda hospitali ya Benjamin Mkapa jijini dodoma

Akizungumza mara baada ya upasuaji kukamilika Septemba 27, 2024 Daktari bingwa wa upasuaji Dkt. Fred Maiko Laizer ,kutokea Mount Meru amesema walipofika katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi wa wilaya ya kiteto walikutana na mgonjwa huyo aliyeandikiwa barua ya rufaa kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa baada ya hospitali hiyo kutokuwa na uwezo wa kutibu tatizo hilo

“ Baada ya Daktari bingwa wa upasuaji kumfanyia vipimo na alizui rufaa hiyo na kumfanyia matibabu hapa hapa kiteto kutokana na uwepo wa vifaa tiba vya kisasa kwa kushirikiana na madaktari wenyeji jambo lilompunguzia adha ya gharama kwa mgonjwa na ndugu zake” Amesema Dkt. Laizer

kwa upande mwingine Dkt. Laizer amesemea uwepo wa madaktari bingwa hao katika hospitali hiyo umeweza kuwafundisha kutumia kwa mara ya kwanza mashine ya usingizi na ganzi madaktari wenyeji.

“Mashine hii ya usingizi na gazi ililetwa na MSD hapa lakini hawakuwahi kuotumia kutokana wahakuwa na ujuzi juu ya mashine hii, hivyo kambi hii ya madaktari bingwa wa Rais Samia imeweza kuwafundisha namna ya kuiwasaha na kuitumia kwa wagonjwa na hadi sasa wameweza kuimaster vizuri na hata tukiondoka wataweza kuendelea kutoa huduma kwa kutumia mashine hii”