Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

PONGEZI PROF. JANABI KWA KUTOA ELIMU JUU YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Posted on: May 16th, 2024

UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA AFYA 2023/24

Na WAF - Dodoma

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya ulaji wa vyakula pamoja na kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa Yasiyoambukiza .

Waziri Ummy ametoa pongezi hizo Bungeni Mei 13, 2024 akiwa anawasilisha hotuba yake ya bajeti ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha 2024/25 akielezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika utoaji wa huduma za Kinga nchini.

"Nitumie fursa hii kuwapongeza wataalam wote kwa kutoa elimu dhidi ya magonjwa Yasiyoambukiza, kipekee nampongeza Prof. Mohamed Janabi kwa jitihada anazozifanya katika kuelimisha jamii kuhusu magonjwa hayo, Tusidharau mafundisho yake na wataalam wengine wa afya." Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara imeendelea kuelimisha jamii kupitia njia mbalimbali kuhusu ulaji unaofaa, kushughulisha mwili, kuacha matumizi ya tumbaku na madhara ya unywaji wa pombe kupita kiasi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.

"Kupitia jitihada hizo jumla ya watu zaidi ya Milioni 11 wamefikiwa na elimu ya kinga dhidi ya magonjwa Yasiyoambukiza ambapo wengi hawakuwa na uelewa juu ya magonjwa hayo." Amesema Waziri Ummy