Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

MAABARA YA KIBONG'OTO ITASAIDIA KUDHIBITI MAGONJWA

Posted on: July 15th, 2022

Na.Catherine Sungura,Siha

Kukamilika kwa Maabara ya Afya ya Jamii ngazi ya 3 ya usalama iliyoko kwenye hospitali maalumu ya magonjwa Ambukizi-Kibong'oto Itachangia katika udhibiti wa kusambaa kwa mgonjwa duniani na hivyo kuimarisha uchumi na usalama wa binadamu.

Hayo yamebainishwa jana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi wakati akiwasilisha taarifa fupi ya ujenzi wa maabara ya kisasa mbele ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt.Philip Isdory Mpango wakati wa ufunguzi wa maabara hiyo iliyoko wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro

Prof. Makubi alisema Ujenzi huo wa maabara ulifanyika kwa awamu mbili na umegharimu jumla ya Biilioni 12.5 inayo jukumu la kutoa huduma za Afya ya jamii na ufuatiliaji wa magonjwa yote yenye umuhimu katika jamii yaliyoaninishwa na Shirika la afya Duniani (WHO) na yale ya mlipuko.

Aidha, alisema maabara hiyo itafanya Ufutiliaji wa usugu wa vimelea kwa dawa zinazotumika kwenye matibabu ya magonjwa mbalimbali na kufanya tathimini ya kiwango cha dawa mwilini.

Kwa upande wa Utafiti Katibu Mkuu huyo alibainisha kuwa maabara hiyo itafanya pia tafiti mbalimbali na ubunifu (innovation) katika sayansi ya tiba na kinga katika ugunduzi wa Dawa, Vitendanishi, Vifaa tiba pamoja na kutengeneza chanjo mbalimbali za kuzuia na kukinga magonjwa ambukizi.

Pia Kutunza vimelea vya magonjwa mbalimbali ikiwemo vinasaba vya vimelea mbalimbali Kutoa mafunzo ya kiuchunguzi na ubunifu kwa wataalamu mbalimbali katika sekta ya Afya.

Hata hivyo alisema maabara hiyo inatarajia kuboresha huduma za tiba ,kupunguza gharama ambazo Serikali inaingia katika kupeleka sampuli nje ya nchi kwa uchunguzi .

Prof. Makubi alisema katika kuimarisha mapambano dhidi ya magonjwa ambukizi mwaka 2016 ,Wizara ilibuni na kuandaa andiko la ujenzi wa mradi mkubwa wa Maabara ya Afya ya Jamii Kibong'oto.

Mradi huo ulikusudiwa kuenzi malengo ya Wizara na Serikaki ya kuipandisha hadhi hospitali ya Kibong'oto kutoka hospitali maalumu ya rufaa ya Kifua Kikuu na kuwa hospitali ya Taifa ya matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi wa magonjwa ambukizi.