Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

KIGAMBONI YATOA DARASA MAPAMBANO YA USUGU WA VIMELEA KUPITIA UFUGAJI WA KUKU BILA DAWA

Posted on: December 7th, 2025

Na WAF – Kigamboni, Dar es Salaam

Jitihada za kupambana na usugu wa vimelea dhidi ya dawa (AMR) zimeendelea kuimarika kupitia programu ya Mashamba Darasa ya Ufugaji wa Kuku wa Nyama Bila Dawa (Broilers), maarufu kama Kigamboni (BFFS) na Somangila (BFFS) ambazo zimeleta mabadiliko makubwa ya ufugaji wa kuku, kwa kuwafundisha wafugaji kutumia mbinu salama, za kisasa na zenye tija bila kutegemea antibiotics.

Hayo yamebainika Desemba 5, 2025 wakati timu ya washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Saba (7) wa Kanda ya Afrika kuhusu uhamasishaji wa udhibiti wa usugu wa vimelea (AMR) ilipotembelea baadhi ya wafugaji wa Kigamboni na kujionea namna mapambano dhidi ya AMR yanavyoanza kwenye ngazi ya jamii hasa katika l uzalishaji wa chakula.

Akiielezea programu hiyo, mmoja wa wanufaika na mwezeshaji wa mafunzo yaliyotolewa na Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani (FAO), Bi. Evelyn Maige, amesema kuwa kila shamba darasa lina jumla ya wafugaji 30 waliopatiwa mafunzo kwa muda wa miezi sita kwa njia ya nadharia na vitendo.

“Mafunzo yalijikita zaidi kwenye biosecurity, uchanganuzi wa rekodi za uzalishaji, utambuzi wa magonjwa, matumizi sahihi ya chanjo, lishe bora, gharama na faida za ufugaji, pamoja na mabadiliko ya tabia kutoka ufugaji wa mazoea kwenda ufugaji bora usiohitaji dawa,” amesema Bi. Evelyn.

Kwa upande wake Muwakilishi wa Serikali kutoka Wizara ya Mifugo Dkt. Gibonce Kayuni amesema lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea wafugaji uwezo wa kuzuia magonjwa kabla hayajatokea, hivyo kupunguza utegemezi wa antibiotics ambao unasababisha ongezeko la usugu wa vimelea (AMR).

“Kupitia biosecurity ya uhakika, usafi, udhibiti wa watu na vifaa, pamoja na chanjo sahihi kwa wakati, wafugaji sasa wanaweza kulinda afya ya kuku bila kutumia dawa,” amesema Dkt. Kayuni.

Aliongeza kuwa baada ya kumaliza mafunzo, wafugaji wa Kigamboni BFFS na Somangila BFFS wamekuwa wataalam wa ufugaji wa kuku wa nyama bila dawa, Mafanikio ambayo yameongeza uzalishaji wenye tija na kulinda afya za walaji.

“Hadi sasa, jumla ya wafugaji 60 wametambuliwa rasmi na Halmashauri ya Wilaya ya Kigambon