Maoni Ya Wateja

Wizara Ya Afya

HUDUMA ZA KLINIKI YA KINYWA NA MENO ZINAPATIKANA HADI NGAZI YA VITUO VYA AFYA

Posted on: February 29th, 2024



-Dawa ya jino sio kung’oa ni kutibu

Na. WAF - Lindi

Kwa juhudi kubwa zinazoendelea kufanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Afya ni pamoja na ununuzi wa Vifaa Tiba ikiwemo X-ray ya Kinywa ambazo zimeshushwa hadi ngazi ya vituo vya Afya, katika Mkoa wa Lindi zipo katika vituo Sita.

Wazir wa Afya Mhe. @ummymwalimu amesema hayo jioni ya jana Februari 29, 2024 akiwa katika Kituo cha Afya cha Mji wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali, Vituo vya Afya pamoja na Zahanati katika Mkoa wa Lindi.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanza kununua vifaa vya X-ray ya kinywa na kuvishusha katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Wilaya na sasa tunaona vifaa hivyo vimeshushwa hadi katika vituo vya Afya.” Amesema Waziri Ummy

Amesema, wagonjwa wote wenye changamoto ya kinywa na meno kwa sasa hawahangaiki tena kwenda katika Hospitali za Rufaa za Mikoa, huduma hizo zinapatikana hadi kwenye vituo vya Afya ambavyo vipo karibu na wananchi.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. ameishukuru Serikali kwa kuboresha huduma za Kinywa na Meno ndani ya Mkoa wa Lindi ambapo amesema ndani ya Miezi Sita wamepata vifaa hivyo na kuvipeleka kwenye vituo vya Afya.

“Tumeagiza vifaa tiba vingine vya X-ray ya kinywa Vitano ambavyo kwa ujumla tutakua na vifaa hivyo 11 na tutavisambaza hadi kwenye Zahanati ambazo zina watu wengi ili kufikia lengo la Serikali.” Amesema Dkt.

Amesema, huduma hizo pia zinapatikana kwenye cliniki tembezi ambapo inawapa fursa wataalamu wa kinywa na Meno kwenda katika maeneo mengine ambayo hayana huduma na kutoa huduma hizo.